Wednesday, October 16, 2024
KAMATI TENDAJI YA MRADI WA SOFF YAKUTANA KUIDHINISHA MPANGO KAZI WA UTEKELEZAJI WA MRADI TANZANIA.
Monday, October 7, 2024
TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MAFUNZO YA MIFUMO YA UANGAZI WA HALI YA HEWA DUNIANI KWA NCHI ZA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI NA KASKAZINI.
7 Oktoba, 2024, Dar es Salaam:
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) imekuwa Mwenyeji wa mkutano wa Mafunzo ya WMO kwa wataalamu wa hali ya hewa kutoka nchi Wanachama wa WMO Kanda ya Afrika Mashariki na Kaskazini. Lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wataalamu wa Hali ya Hewa wanaofanya kazi katika vituo hivyo vya “WMO Regional WIGOS Centres (RWCs)” vya kanda ya Afrika Mashariki na Kaskazini Afrika.
Akifungua rasmi mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheratons,kuanzia tarehe 7-11 Oktoba, 2024, Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Mhe. Jaji Mshibe Ally Bakari alisema suala muhimu kwa Taasisi za Hali ya Hewa za Afrika ni kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa zenye ubora kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuboresha zaidi shughuli zinazofanywa, ikiwa ni pamoja na kuboresha mtandao wa kubadilishana data ili kuboresha zaidi utabiri wa matukio ya hali mbaya ya hewa katika nchi wanachama wa WMO.
Aidha, Jaji Mshibe aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwekeza katika uboreshaji wa miundo mbinu ya huduma za hali ya hewa. Jaji Mshibe aliwashukuru pia WMO na washirika wengine kwa jitihada zao za kuimarisha huduma za hali ya hewa barani Afrika, ikiwemo kuanzisha mfuko wa uwezeshaji wa huduma za uangazi wa hali ya hewa ambapo kupitia jitihada hizo, kiasi cha dola za kimarekani milioni 9 zimeidhinishwa kuboresha huduma za hali ya hewa nchini Tanzania.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa kudumu wa WMO, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, alieleza umuhimu wa kuimairsha uangazi na kuongeza upataikanaji wa data kwa ajili ya kuimairsha utoaji wa tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa. Aidha Dkt. Chang’a alieleza kuwa Tanzania kupitia TMA imejipanga kuendelea kushiriki katika kuongoza na kuwa kinara katika baadhi ya jitihada za kuimarisha huduma za hali ya hewa Barani Afrika. “ Tumejiandaa vyema kuwa mwenyeji wa Mkutano huu mkubwa wa Kikanda, na pia kama mwenyeji wa Kituo cha mfumo wa Kidunia wa kufuatilia vituo vya uangazi wa hali ya hewa kwa nchi za Afrika Mashariki” alisema Dkt. Chang’a. TMA itawasilisha mada zenye kueleza uzoefu wake katika utekelezaji wa jukumu hilo.
Kwa upande wake, Mwakilikishi kutoka WMO alisema kumekuwa na changamoto ya matukio mbalimbali ya Hali mbaya ya Hewa hivyo ushirikiano wetu utasaidia katka kutoa tahadhari za mapema juu ya matukio ya Hali mbaya ya Hewa na tahadhali za mapema”.Alisema, Abubakari Salih Babiker
Washiriki wa mkutano huo wametoka Taasisi za Hali ya Hewa za nchi za Tanzania, Tunisia, Algeria, Egypt, Sudan, South Sudan, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti, Madagascar, Comoros, Sychelles, Mauritius, Morocco, Afrika Kusini na waalikwa kutoka Oman na Sekretarieti ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
Thursday, September 12, 2024
MHE. MWIGULU: SERIKALI ITAENDELEA KUIPA KIPAUMBELE TMA
12 Septemba 2024, Arusha: Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kuahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuipa kipaumbele kwa kuwa huduma za hali ya hewa zinasaidia katika mipango mbalimbali ya maendeleo.
“Wataalam wa hali ya hewa mnafanya kazi nzuri, utabiri unaotolewa hivi sasa ni wa usahihi na umesaidia sana katika masuala ya kiuchumi na kijamii na mipango ya nchi kwa ujumla”. Alizungumza Dkt. Mwigulu alipotembelea banda la TMA katika viwanja vya AICC, Arusha wakati akifunga rasmi Jukwaa la 16 la Ununuzi la Afrika Mashariki.
Matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa ni suala mtambuka kwani husaidia katika mipango na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamiii hususani katika kupunguza madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa kwa umma
Wednesday, September 11, 2024
TMA YASISITIZA UMUHIMU WA MATUMIZI YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KWA WADAU WA UNUNUZI
10 Septemba 2024, Arusha:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa pamoja na kuchangia gharama za upatikanaji wa huduma hizo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi nchini.
Hayo yalizungumzwa na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa katika mada aliyoiwasilisha katika Jukwaa la 16 la Ununuzi la Afrika Mashiriki katika Ukumbi wa AICC, Arusha, linalofanyika tarehe 09 hadi 12 Sepetemba, 2024.
Dkt. Kabelwa alieleza kuwa, kiasi kikubwa cha matumizi ya fedha kinahusisha ununuzi, ni vyema huduma za hali ya hewa zikapewa kipaumbele katika utekelezaji wa Mipango ya Ununuzi na miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ili kuongeza thamani ya fedha katika mradi. “Kwa kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia miradi mingi ikisimama kutokana na madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa, ni muda muafaka sasa wadau wanaohusika kuhakikisha wanatumia huduma hizo wakati wa ubunifu na kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi yao”. Alisisitiza Dkt. Kabelwa.
Aidha, washiriki walijulishwa kwamba, huduma hizo mahsusi zinahitaji kuchangiwa gharama kidogo ambazo ziliwasilishwa rasmi katika hotuba ya Waziri wa Fedha ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2024/25, kifungu cha 158 ilikieleza mapendekezo ya mabadiliko ya kufanya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, sura 157 kuhusu Ada za Hali ya hewa kwa usalama wa uendeshaji wa Miradi ya Ujenzi. Lengo likiwa ni kuongeza tija na ufanisi wa utendaji kazi na kuimarisha usalama wa watu na mali.
Katika hatua nyingine, wataalaam kutoka TMA kupitia maonesho yanayoendelea katika viwanja vya AICC, walieleza pia huduma za hali ya hewa zinahitaji uwekezaji wa miundombinu ya kisasa na gharama kubwa za uendeshaji ili kuwezesha utoaji wa huduma bora, hivyo ni vyema kwa wadau mbalimbali kujitokeza kutumia huduma hizo sambamba na kuchangia gharama kidogo ya huduma mahsusi.
Saturday, September 7, 2024
TMA YAWAKUMBUSHA WAHANDISI KUZINGATIA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI
Monday, August 26, 2024
TANZANIA YAWANOA WATAALAMU WA HALI YA HEWA AFRIKA KUHUSU MATUMIZI YA RADA ZA HALI YA HEWA.
26 Agosti 2024, Mwanza, Tanzania:
Katika kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za Hali ya Hewa barani Afrika, Kitengo cha Elimu na Mafunzo cha Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kinachoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), wameandaa mafunzo mahsusi ya matumizi ya data na taarifa za Rada za Hali ya Hewa. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Malaika,Mwanza, tarehe 26 hadi 30 Agosti 2024.
Akifungua rasmi mafunzo hayo, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb); alieleza lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha zaidi uwezo wa wataalamu wa hali ya hewa na wataalam wengine husika kutoka baadhi ya Nchi za Afika Mashariki na Kusini mwa Afrika katika matumizi bora ya taarifa za Rada za hali ya hewa kwa ajili ya kuboresha utabiri wa hali ya hewa na utoaji wa tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa kwa jamii.
Aidha, alieleza kuwa mafunzo hayo yanaendana na utekelezaji wa mpango ulioasisiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa utoaji wa Tahadhari kwa Wote (Early Warning for All EW4ALL) ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027, pamoja na Sera ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ya ubadilishanaji wa data za hali ya hewa Kimataifa (“WMO Unified Data Policy”). Mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa nchi wanachama wa WMO kanda ya Afrika (WMO RA1) katika kuongeza uwezo unaohitajika zaidi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na tahadhari kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi husika kukabiliana na ongezeko la idadi na ukubwa wa matukio ya hali mbaya ya hewa katika muktadha wa mabadiliko ya hali ya hewa na hivyo kuchangia kuokoa maisha ya watu na mali zao.
Alisisitiza umuhimu wa kufanya uwekezaji wa miundo mbinu ya kisasa ya hali ya hewa kama vile rada, akifafanua kuwa Tanzania imekuwa kilelezo bora katika kufanya uwekezaji huo pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa nchini, na hivyo kuchochea fursa ya kuandaa mafunzo hayo.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa kudumu wa WMO, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hew ana Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, alieleza kuwa TMA imejiandaa vyema kupitia wataalamu wake katika kutoa mafunzo hayo “Wataalamu watakao toa mafunzo ni wabobezi, na kati yao wamepata mafunzo kutoka Marekani na Finland na vilevile ni wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam”. Alisema Dkt. Chang’a.
Kwa upande wake, Mwakilikishi kutoka WMO (Ofisi ya Mafunzo), Bi. Eunjin CHOI aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha mafunzo hayo muhimu ya matumizi ya taarifa na data za rada za hali ya hewa. “Kupitia ushirikiano huu, kwa pamoja tunaweza kuendeleza malengo yetu ya kuboresha huduma za hali ya hewa, si tu kwa Tanzania bali duniani kote”. Alisisitiza Bi. Eunjin.
Tanzania inatoa mafunzo kwa wataalamu wa hali ya hewa kutoka baadhi ya nchi Wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kanda ya Afrika ambao ni Burundi, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Msumbiji, Malawi, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Sudan Kusini, Uganda, Tanzania na Zambia.
Thursday, August 22, 2024
VULI 2024: MVUA ZINATARAJIWA KUANZA KWA KUSUASUA NA KUTAWALIWA NA VIPINDI VIREFU VYA UKAVU.
Dar es Salaam, 22/08/2024;
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za VULI 2024 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka. Akizungumza wakati wa mkutano na vyombo mbalimbali vya habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga alisema maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka ni Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Dkt Chang’a alisema mvua za Vuli kwa mwaka huu 2024 zinatarajiwa kuanza kwa kusuasua zikitawaliwa na vipindi virefu vya ukavu, aliongezea kuwa maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani huku vipindi vya joto kali kuliko kawaida vikitarajiwa.
“Mvua za Vuli kwa mwaka huu 2024 zinatarajiwa kuanza kwa kusuasua,zikitawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wake ukitarajiwa kuwa usioridhisha katika maeneo mengi, ingawa maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani japo izingatiwe kuwa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza katika maeneo machache na vipindi vya joto kali kuliko la kawaida vinaweza kujitokeza”. Alisisitiza Dkt. Chang’a
Akizungumza kuhusu athari zinazotarajiwa kujitokeza, Dkt. Chang’a alisema upungufu wa unyevunyevu kwenye udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi, wadudu na magonjwa ya mazao yanatarajiwa kuongezeka, aliwashauri wakulima kutumia mbinu na teknolojia za kilimo himilivu za kuhifadhi maji na unyevunyevu wa udongo sambamba na kupata ushauri kwa maafisa ugani. Kwa upande wa mifugo alisema upungufu wa mvua unatarajiwa kuathiri upatikanaji wa maji na malisho kwa ajili ya mifugo, hali inayoweza kupelekea kujitokeza kwa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi kutokana na upungufu wa maji na malisho hivyo alishauri jamii kuweka mpango mzuri wa matumizi na uhifadhi wa maji pamoja na malisho.
Utabiri wa msimu wa mvua za vuli 2024 unapatikana katika ofisi zote za TMA nchini pamoja na mitandao ya mawasiliano kama vile TMA online TV, tovuti, blog, facebook na Instagram.
Kwa taarifa zaidi tembelea; https://www.meteo.go.tz/uploads/publications/sw1724321444-Mwelekeo%20wa%20Mvua%20za%20Vuli%202024.pdf
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
Dar es Salaam, Tarehe 05/02/2026; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Masika 202 6 kwa maeneo...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...
-
Dar es Salaam, 22 /0 8 /202 4 ; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za VULI 202 4 kwa maeneo yanayopat...









.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)



.jpeg)

.jpeg)



