Wednesday, October 27, 2021
SEKTA MBALIMBALI ZASHAURIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MVUA ZA MSIMU WA NOVEMBA 2021 HADI APRILI 2022 UNAOTARAJIWA KUJITOKEZA
Tuesday, October 26, 2021
TMA YATOA TUZO KWA WANAHABARI BORA WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA 2021.
Dar es Salaam, Tarehe 26/10/2021
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tuzo kwa wanahabari bora wa taarifa za hali ya hewa 2021, tuzo hizo zimetolewa kwa wanahabari waliofanya vizuri katika kutoa taarifa za hali ya hewa kwa jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Septemba 2020 hadi Julai 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Wakunga na Wauguzi Tanzania – Kibaha.
Tuzo hizo zilitolewa rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani S. Nyenzi katika warsha ya wanahabari inayohusu mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha mwezi Novemba 2021 hadi Aprili 2022, ambaye aliwapongeza washindi wa tuzo hizo na kuwapa hamasa wengine kuendelea kufanya kazi hizo kwa weledi ili ziweze kutambuliwa na Mamlaka na kuwa sehemu ya mchakato wa Tuzo hizo katika wakati ujao.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana na kuwapa hamasa wengine kuendelea kufanya kazi bora zaidi na kuwasilisha taarifa za kazi zenu ili ziweze kutambuliwa na Mamlaka na kuwa sehemu ya mchakato wa tuzo hizo katika wakati ujao”. Alizungumza Dkt. Nyenzi.
Awali wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi alieleza kuwa kwa kipindi kirefu sasa TMA imeendelea kuandaa warsha kwa wanahabari kila inapokaribia kutoa utabiri wa msimu wa mvua, na aliahidi kuendeleza utaratibu huo ili kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa usahihi na kwa wakati.
Utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2021 unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27/10/2021, katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Monday, October 25, 2021
TMA YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA KADA YA HUDUMA SAIDIZI
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za Ufundi TMA, Dkt. Pascal Waniha akizungumza na watumishi wakati akifungua mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.
Watumishi katika TMA wakichangia mada wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za Ufundi TMA, Dkt. Pascal Waniha (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.
Pwani; Tarehe 22 – 23 Oktoba, 2021;
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.
Akizungumza wakati akifungua Warsha ya Watumishi wa Kada ya Huduma Saidizi mgeni rasmi, ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za Ufundi TMA Dkt. Pascal Waniha alisema mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa kuboresha upatikanaji, uelewa na matumizi ya taarifa za hali ya hewa ili kusaidia katika kufanya maamuzi sahihi katika shughuli mbalimbali za kilimo.
“Katika kufanikisha adhima hii, Mamlaka imeona ni vyema kutoa mafunzo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi kwani kutokana na shughuli zenu za kila siku licha ya kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, shughuli zenu za nje ya kazi kama vile bustani na kilimo zimekuwa zikiathiriwa kutokana na hali ya hewa hivyo kupitia warsha hii mtaweza kuelewa huduma mbalimbali zitolewazo na TMA na mtakuwa na jukumu la kusaidia kuzitafsiri, kuzitumia na kuzisambaza taarifa hizi kwa wadau ili waweze kukabiliana na changamoto zinazotokana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa”. Alizungumza Dkt. Waniha.
Awali, wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Dkt. Ladislaus Chang’a, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa TMA alimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TMA kwa warsha hii kwani imekuwa sehemu ya historia na kuwahimiza watumishi kujifunza zaidi na zaidi.
“Kila siku ni fursa, kama tumepewa fursa ya kuwa sehemu ya historia basi sisi wenyewe tunatakiwa tuwe historia kwa namna tunavyoishi na kwa namna tunavyofanya kazi”. Alisema Dkt. Chang’a.
Kwa upande wa watumishi, waliishukuru TMA kwa kuandaa na kuwawezesha kushiriki katika warsha hii ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo ambayo haijawahi kutokea na kuomba mafunzo haya kuwa endelevu.
Friday, October 22, 2021
TMA WAJIPANGA KUTOA UTABIRI KATIKA NGAZI YA WILAYA
Dar es Salaam, Tarehe 21/10/2021
“Utabiri huu wa Msimu utaambatana na utabiri katika ngazi ya Wilaya zilizomo kwenye maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua. Hivyo, nawapongeza sana TMA kwa hatua hii kubwa ya kuongeza wigo wa utoaji utabiri hususani kwa watumiaji wa taarifa za hali ya hewa wa sekta mbalimbali ambao wamekuwa na uhitaji wa taarifa za utabiri wa maeneo madogo madogo kwenye maeneo yao kwa kutumia fursa mbali mbali zilizopo”. Dkt. Buruhani Nyenzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu ya “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Aidha, ili taarifa hizi za utabiri zilizoandaliwa kwa kila wilaya, ziwe na tija iliyokusudiwa tunahitaji kuipatia Mamlaka ushirikiano katika kuhakikisha kwamba taarifa hizi zinawafikia watumiaji wa mwisho kwenye sekta mbalimbali ili kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi. Pia alisema wanapojiandaa kupokea taarifa ya Utabiri wa Msimu wa Mvua za Novemba 2021 hadi April, 2022 ni muhimu sana kila mmoja kufuatilia kwa karibu, kuelewa, kupanga na kukabiliana na hali ya hewa inayotarajiwa katika sekta yake. Aliongezea Dkt. Nyenzi
Kwa upande wake Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) amesema kuwa ni vyema kila wilaya na kila sekta ikatumia taarifa za hali ya hewa katika kufanya maamuzi sahihi na kuweka mipango ili kuboresha huduma zao kwa lengo la kuongeza tija na pia kupunguza athari za hali mbaya ya hewa inapojitokeza.
Aidha, wadau wameipongeza Mamlaka kwa jitihada za kuhakikisha kuwa taarifa hizi za hali ya hewa zinawafikia walengwa wakuu na pia wameitaka Mamlaka kuongeza wigo wa kuifikia jamii ili ipate taarifa kwa wakati na pale inapotokea mabadiliko ya utabiri wa hali ya hewa.
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
06 Septemba 2024, Dar es Salaam: Wahandisi nchini wamekumbushwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa sambamba na kuchangia gharama za upatik...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...