Washiriki wa warsha ya wanahabari kuhusu msimu wa mvua za Vuli, mwezi Oktoba hadi Disemba 2021 katika picha ya pamoja
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakichangia mada katika warsha ya wanahabari kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Disemba 2021) unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 02 Septemba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania |
Kibaha, 1/09/2021.
Ikiwaa ni muendelezo wa ushirikishwaji wa wanahabari katika kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kujadili muelekeo wa msimu wa mvua za VULI kwa mwaka 2021, kabla ya kutolewa rasmi kwa umma Tarehe 02 Septemba 2021.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Agnes Kijazi, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uuguzi, Kibaha – Pwani, Dkt. Ladislaus Chang’a ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya taarifa za hali ya hewa wa TMA aliwahimiza waandishi wa habari kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa TMA kwa umma.
‘Nizidi kuwakumbusha kuwa mabalozi wazuri wa TMA kuelezea na kusisitiza umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii katika shughuli zote za kiuchumi na kimaendeleo. Aliyasema hayo Dr Ladislaus Chang'a.
Dkt. Chang’a alisema kuwa upatikanaji wa taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kwa sababu zina mchango mkubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, nishati, maji n.k. kwani miongoni mwa maeneo yanayopata mvua za vuli, kuna mikoa inayotegemewa katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa nchi na vyanzo vya maji na mabwawa kwa kuzalisha umeme.
Waandishi wa habari wakiwasilisha mada mbalimbali kupitia mkutano huo wameipongeza TMA kwa kuwaongezea uelewa juu ya maswala ya hali ya hewa na kuleta muhitikio kwa vijana kufuatilia taarifa za hali ya hewa.
Aidha, waandishi hao wameahidi kuendeleza ushirikiano mzuri kwa TMA ikiwemo kufuatilia sekta mbali mbali ambazo zinatumia taarifa za hali ya hewa ili kujua namna walivyojipanga kutumia taarifa hizo zinazotarajiwa kutolewa rasmi na TMA ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali mbaya ya hewa.
No comments:
Post a Comment