Dar es Salaam, Tarehe 23, Machi 2021.
Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Prof. Petteri Taalas ametuma Salamu za Pole kwa Tanzania kufuatia Msiba Mkubwa wa Taifa wa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Akimzungumzia Hayati Dkt. Magufuli ameeleza kuwa, Jumuiya ya Kimataifa imeguswa sana na itamkumbuka Rais Magufuli kwa uongozi wake wa mfano, uzalendo, kusimamia utu na kazi kubwa ya kuendeleza amani na kuleta maendeleo ya Nchi yake na Afrika kwa ujumla.
Salamu hizo kutoka kwa Prof. Taalas zimetumwa rasmi kupitia Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
No comments:
Post a Comment