Thursday, August 6, 2020

WANANCHI WA ZANZIBAR WAFURAHISHWA NA NAMNA ELIMU YA HALI YA HEWA INAVYOTOLEWA KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2020.












Matukio mbalimbali kwa picha wakati wageni wakiendelea kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa kutoka kwa wataalam wa hali ya hewa kwenye banda la TMA lililopo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika viwanja vya Dole, Kizambani - Unguja, kuanzia Tarehe 04 - 08 Agosti 2020.

Zanzibar; Tarehe 05/08/2020

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), inashiriki katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Dole, Kizimbani - Unguja, kuanzia Tarehe 04-08 Agosti, 2020, yenye kauli mbiu ya " tudumishe amani na utulivu kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu la Tanzania."

Wageni mbalimbali waliotembelea banda la TMA wameonesha kufurahishwa na namna elimu ya hali ya hewa inavyotolewa bandani hapo na wengi wao wamesisitiza TMA kuendelea kubuni njia nyingine zaidi za kufikisha elimu hiyo kwa wananchi wa visiwani hapo.

Aidha, wataalam wa hali ya hewa toka TMA wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi, usafiri wa anga na maji n.k ili kuelewa namna ya kutumia taarifa za hali  ya hewa kwa usahihi na kuongeza uzalishaji wa malighafi kupitia sekta zao na kujiepusha na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa sambamba na kutambua njia zitumikazo na Mamlaka katika kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa wananchi ikiwemo mitandao ya kijamii.

1 comment:

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...