Sunday, August 9, 2020

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI – ZANZIBAR, BI. MANSURA KASSIM ASISITIZA KUIMARISHA USHIRIKIANO BAINA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA(TMA) NA WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI – ZANZIBAR.

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar, Bi. Mansura Kassim akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa TMA - Zanzibar, Ndg. Mohamed Ngwali mara baada ya kupata elimu ya Sayansi ya hali ya hewa alipotembelea banda la TMA katika maonesho ya NaneNane 2020, Zanzibar

Mkurugenzi wa TMA - Zanzibar, Ndg. Mohamed Ngwali akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar, aliyetembelea banda la TMA katika maonesho ya NaneNane 2020, Zanzibar.













Matukio mbalimbali katika picha wakati wageni kutoka katika sekta mbalimbali wakipata elimu ya sayansi ya hali ya hewa, walipotembelea banda la TMA katika maonesho ya NaneNane 2020, Zanzibar.






Baadhi ya wageni kutoka katika sekta mbalimbali wakipokea zawadi mbalimbali kutoka TMA, walipotembelea banda lake lililopo katika maonesho ya NaneNane 2020, Zanzibar.
 
 
ZANZIBAR, TAREHE 08/08/202

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar, Bi. Mansura Kassim asisitiza TMA na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar kuimarisha zaidi  ushirikiano wa kiutendaji , aliyasema hayo alipotembelea banda la TMA  lililopo katika maonesho ya NaneNane, yanayofanyika katika viwanja vya Dole, Kizimbani – Unguja, kuanzia  tarehe 04 – 08 Agosti, 2020.

“Kutokana na TMA kuwa mdau muhimu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar ni vyema kufanya kazi kwa karibu, japo najua hivi sasa tunashirikiana lakini hapa ninamaanisha kuimarisha  zaidi ushirikiano wetu huku mkitambua kuwa taarifa za hali ya hewa  kama vile hali ya unyevu, mvua, joto na uangazi wa jua zinahitajika sana katika kuendesha mifumo ya kiutendaji (simulation Model) ambayo husaidia kutoa utabiri wa makadirio ya uzalishaji wa mazao.” Alielezea Bi. Mansura Kassim.

Bi. Mansura Kassim aliishauri TMA kutafuta njia ya kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zilizo sahihi zinawafikia wadau kama wakulima na wafugaji kwa wakati ili kupanga mipango yao mapema. Alitolea mfano kuwa wakulima kama wakipata utabiri wa hali ya hewa mapema wanaweza kupanga muda mzuri wa kupiga dawa za kuangamiza wadudu hatarishi kwa mimea bila kuathiriwa na uwepo wa mvua.

Aidha, Mkurugenzi wa TMA - Zanzibar Ndg. Mohamed Ngwali alitolea ufafanuzi moja ya mapendekezo ya Bi. Mansura Kassim juu ya utekelezaji wa majukukumu ya TMA ikiwemo njia zitakazotumika katika usambazaji wa taarifa za hali ya hewa ili kuwafikia watumiaji kwa wakati kwa mujibu wa sheria mpya ya Mamlaka, namba 2 ya mwaka 2019. Kupitia maonesho hayo wageni mbalimbali wameendelea kumiminika katika banda la TMA na kupatiwa elimu ya sayansi ya hali ya hewa.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...