|
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakiwapokea wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020 |
|
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
|
|
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
|
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma akizungumza na menejiment ya TMA walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
|
|
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Suleimani Sarahani Said akizungumza na menejiment ya TMA walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020 |
|
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
|
|
Mkurugenzi Ofisi ya Zanzibar-TMA, Mohamed Ngwali akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020 |
|
Meneja Mipango-TMA, Kidimwa S. Kidimwa akiwasilisha taarifa ya TMA kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020 |
|
Mjumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Ussi Yahya Haji akifuatilia jambo wakati walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020 |
Dar es
Salaam, Tarehe 21/01/2020:
“Iko haja ya
kuangalia ukusanyaji wa mapato ili kusaidia katika uwekezaji mkubwa wa huduma
za hali ya hewa nchini, sisi tutalifuatilia hili ila na nyie muweza kujipanga
vizuri”. Alizungumza Mhe. Hamza Hassan Juma, Mwenyekiti Kamati ya Ardhi na
Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa ziara katika ofisi za Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ambaye aliambatana na wajumbe wengine wa kamati
hiyo.
Mhe. Hamza Hassan Juma alizitaka taasisi zinazotumia
huduma za hali ya hewa kibiashara kuchangia huduma hizo za hali ya hewa kwa
vile huduma hizo zimekuwa zikitumiwa katika kufanikisha shughuli za taasisi
hizo kila siku, huku akitolea mfano wa huduma za bandarini na viwanja vya ndege
ambazo ufanisi wake unategemea kwa kiasi kikubwa huduma za hali ya hewa.
Kwa upande mwingine, Mhe. Hamza Hassan Juma
alifurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na TMA katika kutoa tahadhari za hali
mbaya ya hewa na hivyo kusaidia wananchi kukabiliana na athari zinazoweza
kujitokeza, sambamba na hayo alifurahishwa pia na kuimairishwa kwa muungano kwa
vile Bodi ya TMA hivi sasa ina makamu mwenyekiti anayetokea Zanzibar.
‘Bila Mamlaka ya Hali ya Hewa maisha ya watanzania
yangekuwa ya kubahatisha, huko nyuma watu walikuwa hawafuatilii utabiri wa hali
ya hewa ila kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa (climate change) kumekuwa na
haja ya kujua hali ya hewa itakavyokuwa kwa siku za mbele ili kupanga vyema
shughuli za maendeleo’. Alisema Mhe, Hamza Hassan Juma
Naye makamu
mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Makame
Omar Makame alitoa shukrani za dhati kwa wajumbe waliofika na kuahidi kufanyia kazi mawazo
yaliyotolewa ikiwemo njia za usambazaji taarifa za hali ya hewa kupitia vyombo
vya habari (chaneli) za dini na awali aliwaeleza wajumbe kuhusu mabadiliko ya
TMA kisheria.
Wakati wa ukaribisho na utambulisho Mkurugenzi Mkuu
wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi, aliwakaribisha wajumbe na kuwashukuru kwa kutembelea
TMA kwa mara nyingine tokea mwaka 2017, vile vile aliwasilisha taarifa ya
Mamlaka ambayo iliweza kuonesha huduma mbalimbali za TMA na utekelezaji wa
maagizo yaliyotolewa na kamati hiyo mwaka 2017 ikiwa ni pamoja na kufanikisha
ukarabati wa jengo la ofisi ya TMA, Chukwani, Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati hiyo walifurahishwa na utendaji
wa TMA na kwa umoja wao waliipongeza Mamlaka kwa kazi nzuri wanayofanya katika
kuokoa Maisha ya watu na mali zao. Aidha walitaka TMA kuendelea kutoa elimu (awareness) ili wananchi hasa
wavuvi wazitumie taarifa za hali ya hewa.
‘kila
inapotokea hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya bahari watu wa visiwani hususani
Pemba huwa wanaathirika kwasababu ya ufuatiliaji usioridhisha wa taarifa
zinazotolewa na TMA, kuna haja ya kutoa elimu kwa jamii hadi kufikia ‘level’ ya
familia’ alisema Mhe. Sulemani Sarahani Said makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.
katika kuhitimisha ziara yao wajumbe wa kamati walitembelea
maeneo mbalimbali na kujionea namna kazi kubwa ya kuandaa utabiri inavyofanyika
kwa saa 24, uokozi wa data za hali ya hewa kutoka katika makaratasi (taarifa za
muda mrefu kuanzia 1800) na kuziweka katika mfumo wa kidigitali, usambazaji wa
taarifa za hali ya hewa kupitia studio ya TMA. Huduma hizo za hali ya hewa
zilizoboreshwa ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.
IMETOLEWA
NA
KITENGO
CHA UHUSIANO
MAMLAKA
YA HALI YA HEWA TANZANIA