Mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi na mwakilishi wa Entrerprise Electronics Corporation (ECC) kutoka Marekani bw. Edwin Kasanga wakionyesha mkataba waliousaini |
Mwakilishi wa Entrerprise Electronics Corporation (ECC) kutoka Marekani bw. Edwin Kasanga akiongea kwa niaba ya ECC |
Mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi akiongea mara baada ya kusaini mkataba |
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA dkt.Buruhani Nyenzi naye akiongea mara baada ya kushuhudia utiaji sahini wa mkataba huo |
Baadhi ya wajumbe wa bodi na menejimenti ya TMA wakifurahia jambo mara baada ya kusainiana mkataba |
19/10/2018, Dar
es Salaam.
Katika jitihada za kuzidi kuboresha
huduma za hali ya hewa nchini, Serikali ya awamu ya tano imekamilisha
upatikanaji wa radar ya hali ya hewa ya
tatu kwa kusaini mkataba utakaochukua
miezi kumi na nne (14) mpaka kukamilika kwa radar hiyo. Radar hiyo itafungwa
mkoani Mtwara, Mikindani katika kilima cha Mbae.
Akizungumza wakati wa kusainiana mkataba
huo, mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Dkt. Buruhani Nyenzi amesema kuwa lengo ni kuhakikisha mamlaka inazidi
kujengewa uwezo wa kuendelea kuboresha huduma zake hususani katika kutoa
utabiri sahihi wa hali ya hewa, hivyo upatikanaji wa radar hii ni neema kwa
wananchi wa mikoa ya Kusini mwa
Tanzania. Aidha aliongezea TMA iko katika hatua za mwisho za zabuni ili
kukamilisha ununuzi wa radar nyingine mbili zitakazofungwa Kigoma na Mbeya.
Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt.
Agnes Kijazi aliishukuru serikali kwa jitihada zake za kuboresha huduma za hali
ya hewa nchini kwa kuendelea kukamilisha ahadi ya kufungwa radar saba nchi nzima,
hii ikiwa radar ya tatu baada ya kufungwa kwa radar iliyopo Dar es Salaam na Mwanza.
Naye mwakilishi wa Entrerprise Electronics
Corporation (ECC) kutoka Marekani bw. Edwin Kasanga alihakikishia bodi na
menejiment ya TMA kuwa watamaliza kazi kwa wakati kulingana na makubaliano ya
mkataba ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa radar ya kisasa zaidi.