Friday, August 28, 2015

TAARIFA ZISIZO ZA KWELI ZA UWEPO WA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI KATIKA MAENEO YA DAR ES SALAAM, PWANI, TANGA, UNGUJA NA MTWARA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawatahadharisha wananchi kuhusu taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya Kijamii inayohusu uwepo wa upepo mkali utakao vuma kwa kasi ya km 123.7 kwa saa na mvua kubwa kwa siku ya tarehe 29/08/2015 kuanzia saa 7 mchana.
Taarifa hii si ya kweli na kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) haijatoa TAHADHARI hiyo.
Utabiri sahihi wa kesho tarehe 29/08/2015 katika maeneo hayo ni kama ifuatavyo: Mvua nyepesi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo hayo( Dar es Salaam, Pwani,Morogoro, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba). Upepo unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya wastani wa kilometa 30 kwa saa katika pwani ya kaskazini( Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba) na kwa kasi ya kilometa 20 kwa saa katika pwani ya kusini(Mtwara).
Aidha, Mamlaka inapenda kuujulisha umma kuwa ina utaratibu maalumu wa kutoa tahadhari kwa kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii https://www.facebook.com/tmaservices,https://twitter.com/tma_services, https://www.youtube.com/user/TanzaniaMetAgency, http://tma.meteo.go.tz/cap/en/alerts/rss.xml, http://meteotz1950.blogspot.com/ na tovuti yetu http://www.meteo.go.tz/ hivyo basi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa wito kwa umma kuacha kutoa na kusambaza taarifa za kupotosha katika mitandao ya kijamii. 


Imetolewa na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...