Picha: Mwakilishi
wa Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Warioba Sanya (watatu kutoka kushoto), Mkurugenzi
Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi (wapili kutoka kushoto),Mwakilishi wa Katibu Mkuu
WMO Bw. Samuel Muchemi (wa kwanza kushoto)
na mwenyekiti wa madiwani wilaya ya Sengerema Bw. Ibrahimu Kazungu kwenye
picha ya pamoja na washiriki wa warsha inayohusu uboreshaji wa huduma za hali
ya hewa katika maeneo ya Ziwa Victoria kwa sekta ya wakulima na wafugaji,
wavuvi na wasafirishaji, yenye lengo la kupata mrejesho kutoka kwa jamii
inayoishi Kanda ya Ziwa, kuanzia tarehe 18-20 Agosti 2014 katika hotel ya Gold
Crest-Mwanza
Na. Monica Mutoni
Mamlaka
ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani ilianzisha
huduma ya kutoa taarifa za hali ya hewa hususan tahadhari kupitia simu za
mkononi na vyombo vya habari vya kijamii kama redio, na magazeti. Huduma hiyo ilizinduliwa
rasmi mwaka jana 17 Julai 2013 huko Sengerea mkoani Mwanza na Naibu Waziri wa
Uchukuzi Dkt Charles Tizeba.
Katika
kuhakikisha huduma hii inafanya kazi kwa ufanisi TMA pamoja na WMO wameandaa
warsha inayohusu uboreshaji wa huduma za hali ya hewa katika maeneo ya Ziwa
Victoria kwa sekta ya wakulima na wafugaji, wavuvi na wasafirishaji, yenye
lengo la kupata mrejesho kutoka kwa jamii inayoishi Kanda ya Ziwa, kuanzia
tarehe 18-20 Agosti 2014 katika hotel ya Gold Crest-Mwanza
Akiongea
kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi Bw. Warioba ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa
Mwanza alisema ‘ Huduma hii ni nzuri hasa ikizingatiwa ongezeko la matukio ya
hali mbaya ya hewa katika maeneo ya Ziwa Victoria’ Vilevile aliishukuru WMO kwa
kufadhili huduma hiyo na wananchi wa Wilaya ya Sengerema kuitumia vizuri huduma
hii.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi alisema ‘Katika kuhakikisha TMA inazidi
kuziboresha huduma zake, wataalam wa TMA wameweza kutembelea maeneo mbalimbali
ya Wilaya ya Sengerema ili kujua zaidi majanga yanayoikumbuka wilaya hiyo, hii
itasaidia namna ya uandaaji wa taarifa zinazohitajika na wananchi, aliongezea
‘kwa kupitia mradi huu TMA imeweza kuorodhesha namba za simu za mkononi kwa
wakazi zaidi ya 350, ambapo watu hawa hutumiwa utabiri wa hali ya hewa pamoja
na tahadhari hivyo kuweza kutumia kwa shughuli zao na kusambaziana, vilevile taarifa hizi hutumwa
kwa wasimamizi wa mradi huu wilayani na vyombo mbalimbali vya habari’
Kwa
upande wa WMO, mwakilishi kutoka WMO Bw. Samuel Muchemi alielezea kwa kiufupi
nia ya mradi huo’aliipongeza TMA kwa umakini wake katika kutekeleza mradi huu,
kwa kulinganisha na shukrani na shuhuda zilizotolewa na wavuvi, wakulima,
wafugaji na na wasafirishaji.Aidha warsha itapitia rasimu ya mkataba wa
makubaliano (MoU) na Kanuni za ufanyaji kazi (Standard Operating Procedures)
TMA kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari imejikita katika
kuhakikisha jamii inapata taarifa za hali ya hewa kwa wakati hususan kipindi
cha matukio makubwa yatokanayo na hali mbaya ya hewa kama vile tsunami,mvua
kubwa, ukame, upepo mkali, mawimbi makubwa n.k hivyo kuisaidia jamii
kujihadhari na madhara hayo.
IMETOLEWA
NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.