Dar es Salaam, 25 Oktoba, 2025 Mchana:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoataarifa ya mwenendo wa Kimbunga “CHENGE” katika Bahari ya Hindi, Kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar.
Kimbunga “CHENGE” kimeendelea kusalia baharini nakusogea kuelekea magharibi, huku kikipungua nguvu yake. Hadi asubuhi ya leo kilikuwa katika eneo la Bahari umbali watakribani kilometa 1,280 Mashariki mwa pwani ya kisiwa cha Mafia.
Uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kuwaKimbunga hicho kinatarajiwa kuendelea kusogea kuelekeaMagharibi zaidi mwa Bahari ya Hindi ulipo ukanda wa pwaniwa nchi yetu huku kikiendelea kupungua nguvu yake kadrikinavyosogea. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha uwezekanomdogo wa ongezeko kidogo la kasi ya upepo na mawimbimakubwa ya Bahari kati ya tarehe 26 hadi 28 ya Mwezi Oktoba, 2025 kwa maeneo ya ukanda wa pwani ya nchi yetu. Vilevile, upo uwezekano mdogo wa vipindi vichache vya mvua kubwa kujitokeza hususani katika maeneo ya visiwa vyaUnguja na Pemba pamoja na mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar es salaam na Tanga na maeneo jirani katika kipindi hicho cha tarehe 26 na 28 ya Mwezi Oktoba 2025.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendeleakufuatilia mwenendo wa kimbunga “CHENGE” na athari zakekwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoataarifa kila inapobidi.
USHAURI: Watumiaji wa Bahari na wananchi kwa ujumlawanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wakisekta.

No comments:
Post a Comment