Matukio mbalimbali katika picha wakati wataalam bingwa wa hali ya hewa (Meteorologist) kutoka vituo vya hali ya hewa hapa nchini walipokutana kujadili msimu wa mvua za Vuli, 2020 |
Dar es Salaam, Tarehe; 01/09/2020.
“Napenda kuwahamasisha ninyi wataalam bingwa wa hali ya hewa kufanya tafiti mbalimbali za hali ya hewa zitakazotusaidia kuboresha zaidi utabiri wa hali ya hewa unaoendana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa yanayotukabili mara kwa mara hapa nchini”. Alizungumza Dkt. Kijazi
Alisisitiza hayo Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) alipokuwa akifungua kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu bingwa wa hali ya hewa kutoka katika vituo mbali mbali vya hali ya hewa hapa nchini ili kujadili utabiri wa msimu wa Vuli 2020.
Aidha, Dkt. Kijazi aliwataka wataalam bingwa hao kuhakikisha wanatumia vyema kikao hicho kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutumia utaalamu wao kutoa utabiri wa vuli 2020 na kujadili athari zinazoweza kujitokeza kutokana na utabiri huo. Alisema, athari watakazozijadili zitajadiliwa zaidi katika kikao cha wadau.
Kwa upande wa wataala hao bingwa walioshiriki kikao hicho walishukuru
kufanyika kikao hicho muhimu ikiwa ni
mwendelezo wa maboresho ya utendaji kazi wa pamoja katika kujadili mwelekeo wa
misimu ya mvua. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu-
TMA, Ubungo Plaza.
No comments:
Post a Comment