Tuesday, September 8, 2020

VULI 2020: MAENEO MENGI YA NCHI YANATARAJIWA KUPATA MVUA ZA CHINI YA WASTANI HADI WASTANI.

 



Dar es Salaam, 08/09/2020;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za VULI 2020 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka. Akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi alisema maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka ni Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani ikijumuisha kisiwa cha Mafia Tanga na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma (wilaya za Kibondo, Kakonko na Kasulu).

Dkt Kijazi alisema, mvua za Vuli kwa mwaka huu zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani na zitakazoambatana na vipindi virefu vya ukavu katika maeneo mengi ya nchi, aidha mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza kwa kuchelewa kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Novemba, 2020 katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki, na ukanda wa pwani ya Kaskazini pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.

Akizungumza kuhusu athari zinazotarajiwa kujitokeza, Dkt. Kijazi alisema upungufu wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi, magonjwa ya mlipuko kutokana upungufu wa maji safi na salama, upungufu wa malisho na maji unaweza kujitokeza hivyo uwezekano wa kutokea migogoro kati ya wakulima na wafugaji unatarajiwa.

“Matukio ya moto katika mapori na misitu yanategemewa kutokea, mamlaka husika zinashauriwa kupanga mikakati mahsusi ya kukabiliana na hali hiyo, nitoe angalizo,ingawaje maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadiwastani, izingatiwe kuwa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza yakajitokeza katika maeneo machache”. Aliongezea Dkt. Kijazi

Utabiri wa msimu wa mvua za vuli 2020 unapatikana katika ofisi zote za TMA nchini pamoja na mitandao ya mawasiliano kama vile TMA online TV, tovuti, blog, facebook na Instagram.

Kwa taarifa zaidi tembelea; http://www.meteo.go.tz/uploads/weathers/forecast/en/1599567307-Seasonal%20Rainfall%20Outlook%20OND%202020%20(English%20Version)-FINAL.pdf

Monday, September 7, 2020

TMA YAWAZAWADIA WANAHABARI BORA WA HABARI ZA HALI YA HEWA.






















TMA, Makao Makuu-Dar es Salaam, Tarehe; 07/09/2020.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewazawadia wanahabari waliofanya vizuri katika kuandika habari za hali ya hewa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Septemba 2019 hadi Septemba 2020. Tuzo hizo zilitolewa rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani S. Nyenzi  katika warsha ya wanahabari kuhusu mweleko wa msimu wa mvua za vuli 2020,  ambaye aliwapongeza washindi wa tuzo hizo na kuwataka wanahabari wote kuendelea kuzipa taarifa za hali ya hewa kipaumbele zaidi na wasisite kuziwasilisha kwaajili ya ushindani.

“Shindano kama hili linaleta morali kwenu ninyi na hata kwa wanahabari wengine wasiokuwepo hapa, hivyo niwaahidi tu kuwa huu ni mwanzo na hizi tuzo zitaboreshwa zaidi hapo mbeleni na kuongeza ushindani, hivyo mjipange katika hilo”. Alizungumza Dkt. Nyenzi, Mgeni Rasmi wa tuzo hizo na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA.

“Hata kama TMA haijawaita kufanya kazi kwa mwaliko rasmi  basi nyie mtumie weledi wenu kuzitafuta sehemu za kuzungumzia kwani ziko nyingi sana”. Aliongeza Dkt. Nyenzi. 

Awali wakati akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi alieleza kuwa ili kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinaifikia jamii kwa wakati na usahihi, Mamlaka imekuwa  ikitumia njia mbalimbali ikiwemo wanahabari ambao ni daraja muhimu katika kuwafikia wananchi wote. 

“Katika kuonesha umuhimu wa tasnia hii, Tarehe 3 mwezi huu, Mamlaka ilikutana na wadau wa sekta zingine na baadhi yenu mlishiriki katika mkutano huo, lakini leo tumeamua kuwa na mkutano huu ambao ni mahususi kwa wanahabari peke yenu”. Alisema Dkt. Kijazi

Kwa upande wa mshindi wa kwanza wa tuzo hizo, Bi. Theopista Nsanzugwako kutoka gazeti la Habari Leo alitoa wito kwa wanahabari kuilisha jamii taarifa za hali ya hewa  ili wananchi waweze kuzitumia katika kukabiliana na hali ya hewa husika, kwa vile hali ya hewa ni maisha.

Naye mshindi wa pili wa tuzo hizo, Bw. Jerome Risasi kutoka Clouds Media aliwahimiza wanahabari kufuatilia mara kwa mara taarifa za hali ya hewa zinazotolewa ili wananchi wapate taarifa za uhakika ikiwa ni pamoja na kujua athari za hali ilitolewa.

Lengo kuu la warsha hiyo lilikuwa kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2020 ili kupata uelewa wa pamoja na kurahisisha uwasilishwaji wake kwa jamii katika lugha inayoeleweka, pamoja na kuwapongeza wanahabari waliofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja



















 





Friday, September 4, 2020

TMA YASISITIZA MATUMIZI YA TAARIFA MAHUSUSI ZA HALI YA HEWA KWA MAENDELEO YA UCHUMI WA VIWANDA.

Mgeni rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi akizungumza kwa kusisitiza wakati akifungua warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi  akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa  akiongea kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi katika warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania











Wadau mbalimbali kutoka sekta ya Kilimo, Mifuko  Nishati, Maafa, Afya, Habari, Maji, Uvuvi, Taasis zisizo za Serikali (NGO's) n.k wakichangia mada katika warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania







Wadau mbalimbali kutoka sekta ya Kilimo, Mifuko  Nishati, Maafa, Afya, Habari, Maji, Uvuvi, Taasis zisizo za Serikali (NGO's), n.k wakiwa katika makundi wakijadili athari na ushauri kwa msimu wa mvua za Vuli 2020 katika warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania








Wadau mbalimbali kutoka sekta ya Kilimo, Mifuko  Nishati, Maafa, Afya, Habari, Maji, Uvuvi,  Taasis zisizo za Serikali (NGO's), n.k zilizopo hapa nchini wakiwasilisha athari na ushauri katika sekta zao kwenye warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania




Matukio kwa picha wakati wadau wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa katika warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania


Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi kwenye warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2020 unaotarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 08 Septemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania

Dar es Salaam, Tarehe; 03/09/2020.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeweka msisitizo wa matumizi ya taarifa mahususi za hali ya hewa kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda. Hayo yalizungumzwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa utabiri wa mvua za vuli 2020, uliofanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania), Dar es Salaam.

 “Taarifa za hali ya hewa zinalenga kusaidia katika kufikia malengo ya Mpango wa Taifa katika kujenga uchumi wa viwanda. Kwa mfano, katika eneo la uzalishaji mazao ya chakula na biashara, Nishati na maji; huduma za hali ya hewa zikitumika ipasavyo tutajihakikishia upatikanaji wa malighafi na nishati kwa viwanda vyetu”. Alizungumza Dkt. Nyenzi, Mgeni Rasmi katika mkutano huo na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA.

“Ni matumaini yangu kuwa mkutano wa leo utakuwa ni hatua muhimu kuelekea mashirikiano ya kisekta kati ya Mamlaka ya Hali ya Hewa na watumiaji wa huduma za hali ya hewa na hivyo kuongeza matumizi ya huduma hizo kwa  maendeleo endelevu. Kila mmoja wetu ana mchango na jukumu la kufuatilia kwa karibu, kuelewa na kukabiliana na hali ya hewa ilivyo leo na itakavyokuwa siku zijazo. Tuendelee kuelimishana kupitia njia zote stahiki kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na namna ya kukabiliana nayo na wakati huohuo tukiendelea kutekeleza sera ambazo zitatusaidia sasa na siku zijazo”. Aliongeza Dkt. Nyenzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi alisisitiza kuwa kuna uhusiano mkubwa wa hali ya hewa na uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda pamoja na ujenzi wa viwandavyenyewe. Hivyo alieleza umuhimu wa kutumia taarifa za hali ya hewa katika uchumi wa viwanda. Alieleza kwamba Mamlaka imeanzisha huduma za utoaji taarifa mahususi kwa matumizi katika sekta mbalimbali. Maandalizi ya taarifa hizo yanahusisha ushirikiano na wadau husika, ambapo wadau katika sekta ya utalii na madini wameanza kunufaika.

Mamlaka imedhamiria kuendelea kuandaa taarifa za aina hiyo kwa kushirikiana na wadau wa sekta nyingine. Natoa wito kwa wadau mliopo hapa tuendelee kushirikiana katika kuandaa taarifa katika sekta zenu. Wakati huo huo tukizingatia utekelezaji wa sheria Na. 2 ya 2019 iliyoanzisha Mamlaka ya Hali ya Hewa ambayo imeweka bayana mahitaji ya wadau wa sekta mbalimbali ”. Alisema Dkt. Kijazi

Naye mdau kutoka Wizara ya Kilimo Bi. Halima Kwikwega aliungana na wadau wengine kuipongeza TMA kwa kazi nzuri ya kutoa utabiri ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa na uhalisia wa hali ya juu, vilelvile alieleza kufurahishwa na maandalizi yanayofanywa na TMA katika kuandaa mikutano kama hii na kuahidi kuendelea kutumia utabiri unaotolewa kwa manufaa ya sekta ya kilimo na nchi kwa ujumla. Alisema ni muhimu kuzingatia kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa letu, akitolea mfano utabiri wa msimu uliopita uliwasaidia wakulima kupata mavuno yakutosha na hivyo kuongeza tija katika uchumi wa Taifa letu. 

Wadau wengine kutoka sekta mbalimbali ikiwemo Wizara ya Kilimo – Zanzibar, TANESCO, Vyombo vya Habari, TPDC, Red Cross, Mifugo na Uvuvi, Shirika la Chakula Duniani (FAO) n.k waliipongeza TMA kwa utabiri wa uhakika ambao umeongeza tija katika sekta zao.

Lengo la mkutano huo wa kikazi ni kuongeza mchango wa wataalam juu ya matumizi ya taarifa za hali ya hewa na athari zinazotarajiwa katika sekta mbalimbali, kukusanya maoni na ushauri kutoka katika makundi ya wadau yanayotumia taarifa za hali ya hewa pamoja na  kuongeza uelewa wa wadau na jamii kwa ujumla juu ya tafsiri bora na sahihi za utabiri wa mvua za vuli  kwa sekta mbalimbali. Utabiri wa mvua za vuli utatolewa rasmi tarehe 8/9/2020.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...