Mwezeshaji Bw. Augustine Kanemba akimkaribisha mwakilishi kutoka WMO, Dkt. Elijah Mukhala kutoa nasaha zake katika warsha hiyo.
Mkurugenzi Mkuu TMA akitoa hotuba fupi wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuhutubia wanawarsha
Mgeni rasmi Brigedia jenerali Mbazi Msuya akihutubia wakuu wataasisi zinazomiliki vituo vya hali ya hewa wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya wanawarsha wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha waliokaa kutoka kulia kwa mgeni rasmi ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Kijazi, mkurugenzi kitengo cha usalama wa chakula, Kilimo Bw. Ombaeli Lemweli na mkurugenzi mkuu TANAPA Dkt. Allan Kijazi kutoka kushoto kwake ni mwakilishi wa WMO akifuatiwa na mkurugenzi wa huduma za utabiri TMA Dkt. Hamza Kabelwa.
KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI
MKUU AAGIZA TAASISI ZINAZOMILIKI VITUO VYA HALI YA HEWA NCHINI KUSHIRIKIANA
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) wameandaa warsha ya siku moja ya wakuu wa taasisi zinazomiliki vituo vya
hali ya hewa hapa nchini. Warsha hiyo ilifanyika katika hotel ya Kibo Palace
mjini Arusha tarehe 30 April, 2015. Akifungua warsha hiyo Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa kamati inayosimamia utekelezaji wa ‘Global
Framework for Climate Services (GFCS)’ Dkt. Florence Turuka aliwaagiza wakuu
hao wa taasis kushirikiana ili kuimarisha uwezo wa nchi
katika kukusanya takwimu za hali ya hewa, kutoa tahadhari ya mapema ili kupambana
na athari za mabadiliko ya tabia nchi.‘madhumuni ya warsha ni kujadiliana na
kukubaliana namna bora ya kushirikiana juu ya ubadilishanaji wa taarifa na
takwimu kutoka katika mitandao ya vituo vya hali ya hewa ili kutumia taarifa
hizo ipasavyo katika shughuli mbali mbali za uchumi kwa ustawi wa jamii. Aidha,
taarifa hizo zitasaidia katika kukabiliana na majanga yatokanayo na hali mbaya
ya hewa nchini ambayo ni muhimu kwa kuokoa maisha ya watu na mali zao.’ alizungumza
Dkt. Turuka
Kwa upande wake Dkt. Agnes
Kijazi, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na mwakilishi wa
kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni (WMO),
aliwashukuru wakuu wa taasis zinazomiliki vituo vya hali ya hewa hapa nchini
kwa kukubali kuhudhuria warsha hiyo. Dr. Kijazi aliongeza kwamba warsha hiyo ni
muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa ‘WMO Integrated Global Observing
System (WIGOS)’ hapa nchini. ‘Suala moja muhimu litakalojadiliwa katika warsha
hii ni mkakati wa utekelezaji wa mpango wa WIGOS hapa nchini, mapendekezo
yatakayotolewa katika warsha hii yatasaidia kutoa mwelekeo wa jinsi gani
tutakavyotekeleza mpango wa WIGOS na Global Framework for climate services
(GFCS) hapa nchini’ aliongeza Dkt Kijazi.
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI OFISI YA UHUSIANO- TMA
No comments:
Post a Comment