Mgeni rasmi Dkt. Kijazi akiongea na wana warsha katika ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Wanawarsha wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mgeni rasmi akifunga warsha ya siku moja ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wanawarsha wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha wadau wa sekta mbalimbali nchini
wananufaika na huduma za hali ya hewa katika shughuli zao za kila siku.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes kijazi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi
alielezea umuhimu wa mkakati huo wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa hali
ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni
ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya
Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
‘TMA kwa kipindi cha miaka
ya hivi karibu imekuwa ikikutana na wadau wa sekta mbalimbali na kupata maoni
yao juu ya huduma zinazotolewa (user engagement) na vilevile kubadilisha namna
ya uhifadhi wa takwimu za hali ya hewa (data rescue and digitization), kwa
kupitia maoni hayo Mamlaka imeona ni wakati muafaka kuwakutanisha wataalamu wa
hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali ili kujadili na kupata suluhisho la
kuboresha huduma zetu’, alisema Dkt. Kijazi.
Mamlaka imekuwa
ikishirikiana na taasisi za kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha utoaji wa
huduma zake unakidhi matakwa ya wadau. Katika kutimiza hilo tarehe 11 Novemba
2014 TMA ilisaini makubaliano ya kushirikiana katika kutelekeza baadhi majukumu
yake na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambapo mambo makuu yalikuwa ni
kuhakikisha watumiaji wa huduma za hali ya hewa nchini wanaridhika na huduma
zitolewazo na vilevile kuboresha mfumo wa kuhifadhi takwimu za hali ya hewa.
Katika mkutano huu ambao
umewahusisha pia wakuu wa kanda kutoka TMA na wasimamizi wa vituo vya hali ya
hewa-kilimo vinavyoendeshwa na Mamlaka vilivyopo nchini,washiriki watapata
fursa ya kujadili na kutolea maamuzi maoni ya wadau wa sekta ya kilimo,
nishati, maji, afya na habari na pia kujipanga katika kuwafikia wadau wengine.
IMETOLEWA NA MONICA MUTONI, OFISI YA UHUSIANO TMA
No comments:
Post a Comment