Friday, October 19, 2018

SERIKALI YAZIDI KUIJENGEA UWEZO TMA KWA KUKAMILISHA UNUNUZI WA RADAR NYINGINE YA HALI YA HEWA

Mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi  na mwakilishi wa ECC kutoka Marekani wakisaini mkataba wa radar ya hali ya hewa itakayofungwa Mtwara, shughuli hiyo ikishuhudiwa na mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA dkt.Buruhani Nyenzi na wanasheria kutoka TMA na ECC
Mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi na mwakilishi wa Entrerprise Electronics Corporation (ECC) kutoka Marekani bw. Edwin Kasanga wakionyesha mkataba waliousaini
Mwakilishi wa Entrerprise Electronics Corporation (ECC) kutoka Marekani bw. Edwin Kasanga akiongea kwa niaba ya ECC
Mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi akiongea mara baada ya kusaini mkataba
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA dkt.Buruhani Nyenzi naye akiongea mara baada ya kushuhudia utiaji sahini wa mkataba huo
Baadhi ya wajumbe wa bodi na menejimenti ya TMA wakifurahia jambo mara baada ya kusainiana mkataba



19/10/2018, Dar es Salaam.



Katika jitihada za kuzidi kuboresha huduma za hali ya hewa nchini, Serikali ya awamu ya tano imekamilisha upatikanaji wa radar  ya hali ya hewa ya tatu  kwa kusaini mkataba utakaochukua miezi kumi na nne (14) mpaka kukamilika kwa radar hiyo. Radar hiyo itafungwa mkoani Mtwara, Mikindani katika kilima cha Mbae.



Akizungumza wakati wa kusainiana mkataba huo, mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Buruhani Nyenzi amesema kuwa lengo ni kuhakikisha mamlaka inazidi kujengewa uwezo wa kuendelea kuboresha huduma zake hususani katika kutoa utabiri sahihi wa hali ya hewa, hivyo upatikanaji wa radar hii ni neema kwa wananchi wa mikoa ya Kusini  mwa Tanzania. Aidha aliongezea TMA iko katika hatua za mwisho za zabuni ili kukamilisha ununuzi wa radar nyingine mbili zitakazofungwa Kigoma na Mbeya.



Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi aliishukuru serikali kwa jitihada zake za kuboresha huduma za hali ya hewa nchini kwa kuendelea kukamilisha ahadi ya kufungwa radar saba nchi nzima, hii ikiwa radar ya tatu baada ya kufungwa kwa radar  iliyopo Dar es Salaam na Mwanza.



Naye mwakilishi wa Entrerprise Electronics Corporation (ECC) kutoka Marekani bw. Edwin Kasanga alihakikishia bodi na menejiment ya TMA kuwa watamaliza kazi kwa wakati kulingana na makubaliano ya mkataba ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa radar ya kisasa zaidi.

Thursday, October 18, 2018

MVUA ZA MSIMU: TMA YATOA UTABIRI KWA MAENEO YANAYOPATA MSIMU MMOJA WA MVUA

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) dkt. Agnes Kijazi, mbele ya waandishi wa habari  akichambua  mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua
Wajumbe wa bodi ya ushauri wa Mamlaka (TMA) wakiongozwa na mwenyekiti wa bodi hiyo dkt. Buruhani Nyenzi wakifuatilia uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua.
Baadhi ya waandishi walioshiriki mkutano wa wanahabari wa kutoa mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu kuanzia mwezi Novemba, 2018 hadi Aprili, 2019 katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za TMA. Mkutano huo uliudhuriwa na wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa TMA wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi
Taarifa hiyo inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua (kanda ya magharibi, kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo yaliyoko kusini mwa mkoa wa Morogoro) katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2018 hadi Aprili, 2019. Aidha, taarifa imeendelea kwa kutoa mrejeo wa mvua za Vuli katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria, pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini-mashariki.
Vile vile, ushauri na tahadhari umetolewa kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na wanyamapori, maliasili na utalii, uchukuzi na mawasiliano, nishati na maji, mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa. Kusoma zaidi ingia humu http://www.meteo.go.tz/pages/climate-outlook-for-msimu-rains-nov-2018-apr-2019


Thursday, October 11, 2018

TMA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MVUA ZA MSIMU WA NOVEMBA 2018 HADI APRILI 2019

Pichani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a akifungua rasmi warsha iliyowajumuisha wataalamu wa hali ya hewa TMA na wadau toka Sekta mbalimbali kujadili mvua za msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019

Mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA akiwasilisha mada



Pichani ni wadau kutoka katika sekta mbalimbali wakitoa maelezo ya mchango wa taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao.






Pichani ni Makundi mbalimbali yakijadili namna wanavyoweza kuutumia Utabiri wa Hali ya Hewa katika utekelezaji wa majukumu katika sekta mbalimbali hapa nchini na baadae kuwasilisha kwa wajumbe
Katikati ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa dkt. Ladislaus Chang'a kwenye picha ya pamoja na washiriki kwenye warsha ya wadau kutoka sekta mbalimbali walipokutana na wataalamu wa hali ya hewa kujadili mvua za msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019  


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo tarehe 11/10/2018 imekutana na wadau kutoka sekta ya maafa, afya, kilimo, nishati, mazingira,mipango miji na wanahabari kujadili matarajio na mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 ili kuongeza uelewa wa taarifa za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali zinazoathirika zaidi na hali ya hewa.

Aidha, wadau walipata nafasi ya kujadili mwenendo wa utabiri wa msimu wa vuli (Oktoba hadi Desemba 2018) uliotolewa 05 Septemba 2018 ambao unaonesha kuwa mvua zimeanza (onset) kama ilivyotabiriwa kwa maeneo mengi ingawaje mtawanyiko wake bado haujaimarika hali inayosababishwa na mgandamizo mdogo wa hewa uliopo Mashariki mwa Pwani ya Somalia unaoathiri mifumo ya hali ya hewa

Kwa upande wa mdau kutoka wizara ya afya bw.Stephen Kiberiti aliwashukuru TMA kwa utaratibu wa kukutana na wadau hii inasaidia sekta husika kujiandaa na athari zinazoweza kujitokeza.

Mikoa inayopata mvua mara moja kwa mwaka ni Dodoma, Singida, Katavi, Mbeya,Tabora, Kigoma(ukitoa Kigoma Kaskazini), Mtwara, Lindi,Ruvuma, Iringa, Songwe, Rukwa, Njombe na Kusini mwa Morogoro

Warsha hii imedhaminiwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kupitia mradi wa mfumo wa kidunia wa huduma za hali ya hewa Duniani (Global Framework for Climate Service-GFCS)

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...