Wednesday, September 3, 2025

TMA YAKABIDHIWA RASMI HATI NA: DSMT1086126 YA ENEO LAKE LA KIPAWA



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo ya Sayansi ya Mabadiliko ya hali ya Hewa Duniani (IPCC) Dkt. Ladislaus B. Chang'a amekabidhiwa rasmi hati  ya Kiwanja namba 173 chenye ukubwa wa mita za mraba 10,280 kilichopo Kipawa Wilayani Ilala, Dar es Salaam,tarehe 01/09/2025. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ya Msajili wa Hati Kanda ya Mashariki Adv. Burton Rutta zilizopo Kivukoni, Dar es Salaam. Dkt. Chang'a aliishukuru  Ofisi ya Msajili wa Hati kwa ushirikiano uliotolewa na watumishi wa ofisi hiyo katika kufanikisha upatikanaji wa hati hiyo muhimu kwa TMA na Serikali kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...