Wednesday, August 7, 2024

DKT. CHANG'A AMESHIRIKI KATIKA UTOAJI ELIMU YA SAYANSI YA HALI YA HEWA KWENYE MAONESHO YA NANENANE 2024







Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a ameshiriki katika utoaji wa elimu ya sayansi ya hali ya hewa kwenye maonesho ya NaneNane 2024 katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.

Dkt.Chang'a aliungana na wataalam wengine wa TMA katika muendelezo wa utoaji huduma za hali ya hewa nchini.

Aidha, Dkt. Chang'a alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi.

Mamlaka inaendelea kuwakaribisha wananchi wote kufika kwenye banda la TMA, NaneNane Kitaifa.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...