Monday, April 3, 2023

RAMADHANI OMARY ACHAGULIWA KATIBU WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TMA

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wamemchagua Ndg. Ramadhani Omary kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa TMA, kupitia kikao cha Baraza hili kinachoendelea Morogoro tarehe 03 na 04 Aprili 2023. Ndg. Ramadhani Omary alichaguliwa kwa kupata kura 62 akifuatiwa na Katibu Msaidizi Bi. Mecklina Merchades kura 32, jumla ya kura zilizopigwa ni 94. Katika hatua nyingine, Baraza hilo lilitambulisha wimbo wa TUGHE-Taifa na kuzinduarasmi kipeperushi maalumu na bango la TUGHE-TMA ambavyo vitatumika katikakuitangaza TUGHE-TMA kwenye majukwaa mbalimbali kupitia dhana ya uzalendo, ubunifuna uwajibakaji. Ndg. Ramadhani Omaryni Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka Ofisi ya Kituo Kikuu cha Utabiri, dawati la utabiri wa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...