Thursday, December 22, 2022

TMA YAWAHAKIKISHIA HUDUMA BORA NA UFANISI WADAU WA USAFIRI WA ANGA










Matukio mbalimbali katika picha wakati mkutano na wadau wa usafiri wa Anga ukiendelea katika ukumbi wa TAA, Dodoma tarehe 21 Disemba 2022.


Dodoma; Tarehe 21 Disemba, 2022;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau  wa usafiri wa  Anga wa jijini Dodoma katika ukumbi wa TAA,Dodoma tarehe 21 Disemba, 2022,ili  kujadili maendeleo na mahitaji ya huduma za Hali ya Hewa kwa usafiri wa Anga.


Akifungua mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema “Kusudi la mkutano huu ni kutathimini maendeleo na mahitaji ya utoaji wa huduma za Hali ya Hewa kwa ajili ya usafiri wa Anga ili kuongeza tija na ufanisi katika shughuli na kuhakikisha  usalama wa usafiri wa  Anga ”.Alisema Dkt. Ladislaus Chang’a.


“TMA imeendelea kutambua umuhimu wa mikutano hii kwani imesaidia kuboresha sio tu ubora wa bidhaa zetu  bali pia taratibu za utoaji wa huduma katika sekta ya usafiri wa  Anga. Nakumbuka, miaka ya nyuma kulikuwa na malalamiko kadhaa juu ya kutafuta njia bora ya kuhakikisha taarifa za Hali ya Hewa kwa marubani zinapatikana kwa njia ya mtandao yaani (online), TMA tulifanyia kazi malalamiko hayo na kuweza kutengeneza mfumo wa Tehama wa usambazaji wa taarifa hizo unaoitwa MAIS na kuanza kufanya kazi rasmi mwaka 2012.” Aliongeza Dkt. Ladislaus Chang’a.


Dkt. Chang’a alisisitiza kuwa TMA inafanya kazi kwa kuzingatia taratibu za Kitaifa na Kimataifa. Akizungumzia kuhusu taratibu za Kimataifa, alieleza kuwa TMA imeendelea kukaguliwa kila mwaka na kuendelea kushikilia cheti cha ubora ISO 9001: 2015 na hivyo kuhakikishia ubora wa huduma zitolewazo kukidhi viwango vya Kimataifa.

Na kuhusu mabadiliko ya tabia ya Nchi, TMA imeendelea kufuatilia kwa karibu changamoto ya mabadiliko ya Hali ya Hewa hususan ongezeko la joto na matukio ya hali mbaya ya Hewa ambayo pia yanaendelea kuathiri huduma katika sekta ya usafiri wa Anga na hivyo kuhitaji uimarishaji wa utoaji na matumizi ya taarifa za Hali ya Hewa.


Awali wakati akifungua Mkutano huo, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya Hali ya Hewa kwa kufanya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kisasa vya hali ya hewa ikiwemo Rada.



No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...