Friday, December 30, 2022

TMA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA TANDALE.

 

Dar es Salaam, Tarehe 28/12/2022.

Tunapoelekea katika sherehe za kumaliza mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitembelea kituo cha afya cha Tandale, Tarehe 28/12/2022 na kutoa msaada wa vifaa tiba ambavyo viliwasilishwa rasmi  na Kaimu Meneja wa Masoko wa TMA Bi Monica Mutoni kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a.

Akizungungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Bi. Monica Mutoni alisema msaada wa vifaa tiba hivyo ni matokeo ya Kongamano la 15 la  EUMETSAT lililofanyika mwezi Septemba 2022 kwa lengo la kutoa huduma ya kwanza kwa wadau wa Kongamano hilo kutoka nchi zote za Afrika na baadhi ya nchi za nje ya Afrika.

“vifaa hivyo vilikabidhiwa TMA na wataalamu wa afya kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili, vipo takribani 25, hivyo basi kwa upendo wetu kwenu na kwa kuwa moja ya majukumu ya TMA ni kurudisha kwa jamii, Kaimu Mkurugenzi Mkuu ametuagiza kutoa msaada wa hivi ili kuweza kusaidia jamii na wahitaji wote wanaotumia kituo hiki”. Alisisitiza Bi. Monica Mutoni

Aidha, vifaa hivyo vilipokelewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Tandale, Dkt. Merina Kulwa, ambaye aliishukuru TMA na kusema kuwa msaada huo utasaidia katika kuboresha utoaji huduma kituoni hapo.


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...