Dkt.
Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa,Mwakilishi wa Kudumu
wa Tanzania Katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Mjumbe wa “WMO
Excecutive Council” na Bw. Wilbert Timiza Muruke, Meneja Mahusiano ya Kimataifa
wa TMA katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kamati Kuu ya Shirika
la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Excecutive Council-68) unaondelea, Geneva, Uswisi
kuanzia tarehe 15-24 Juni 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi alikuwa miongoni mwa
wajumbe 37 wa Mkutano wa Sitini na Nane wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Shirika la
Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization Executive Council
WMO-EC 68) unaofanyika makao makuu ya Shirika hilo, Geneva nchini Uswisi
kuanzia tarehe 15 hadi 24 Juni, 2016. Pia Dkt. Kijazi anaingia katika Kamati
Kuu ya WMO akiwa kati ya wanawake wawili (2) kutoka Afrika na watano (5) kati
ya thelathini na saba (37) kuwakilisha Dunia nzima.
Mkutano wa WMO-EC-68
pamoja na masuala mengine unajadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma
za hali ya hewa Duniani sambamba na kutimiza Makubaliano ya Kikanda na
Kimataifa katika kukabiliana na athari zinazosababishwa na mabadiliko ya hali
ya hewa na tabia nchi.
Aidha masuala
yanayojadiliwa ni sehemu ya Mpango Mkakati wa WMO na vipaumbele vyake katika
kipindi cha mwaka 2015-2019 unaojumuisha utekelezaji wa programu za utoaji wa
huduma bora zaidi za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for Climate
Services”, Utekelezaji wa programu ya uboreshaji wa vituo vya upimaji wa hali
ya hewa na ubadilishanaji wa data za hali ya hewa “WMO Integrated Global Observing
System and Information System (WIGOS/WIS), utoaji wa tahadhari za mapema ili
kukabiliana na maafa “Disaster Risk Reduction, Resilience and Prevention”, Uboreshaji wa
huduma za usalama na usafiri wa anga “Aviation meteorological services”,
Kuboresha huduma za hali ya hewa kwa maeneo ya Dunia yenye barafu ya asili
ikiwa ni pamoja na milima mirefu kama Kilimanjaro “Polar and high mountain
regions”, Kujenga uwezo wa rasilimali watu na vitendea kazi hasa kwa nchi
zinazoendelea na visiwa vidogo na tafiti za hali ya hewa. Aidha Mkutano huu
unajadili pia namna ya kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa kama njia
ya kuboresha huduma za hali ya hewa kote duniani na kutatua changamoto za athari
zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi na uhifadhi wa
mazingira.
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI-AFISA UHUSIANO TMA
No comments:
Post a Comment