Wednesday, April 22, 2015

TMA YAJIKITA KATIKA KUKIDHI MATAKWA YA WADAU WA SEKTA MBALIMBALI

Mkurugenzi wa utafiti na matuzi wa TMA Dkt. Ladislaus Chang'a akimkaribisha mkurugenzi mkuu Dkt. Agnes Kijazi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mgeni rasmi Dkt. Kijazi akiongea na wana warsha katika ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.

Wanawarsha wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mkurugenzi mkuu na wakurugenzi wa divisheni sambamba na wanawarsha wengine wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa na watoa mada (pichani hapo juu)
Mgeni rasmi akifunga warsha ya siku moja ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wanawarsha  wa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015. 



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha wadau wa sekta mbalimbali nchini wananufaika na huduma za hali ya hewa katika shughuli zao za kila siku. Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes kijazi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi alielezea umuhimu wa mkakati huo wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali vya TMA waliokutana ili kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta za kilimo, afya, maji, na nishati katika ukumbi wa hoteli ya Bluepearl, Dar es Salaam tarehe 21 Aprili 2015.

‘TMA kwa kipindi cha miaka ya hivi karibu imekuwa ikikutana na wadau wa sekta mbalimbali na kupata maoni yao juu ya huduma zinazotolewa (user engagement) na vilevile kubadilisha namna ya uhifadhi wa takwimu za hali ya hewa (data rescue and digitization), kwa kupitia maoni hayo Mamlaka imeona ni wakati muafaka kuwakutanisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali ili kujadili na kupata suluhisho la kuboresha huduma zetu’, alisema Dkt. Kijazi.

Mamlaka imekuwa ikishirikiana na taasisi za kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha utoaji wa huduma zake unakidhi matakwa ya wadau. Katika kutimiza hilo tarehe 11 Novemba 2014 TMA ilisaini makubaliano ya kushirikiana katika kutelekeza baadhi majukumu yake na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambapo mambo makuu yalikuwa ni kuhakikisha watumiaji wa huduma za hali ya hewa nchini wanaridhika na huduma zitolewazo na vilevile kuboresha mfumo wa kuhifadhi takwimu za hali ya hewa.

Katika mkutano huu ambao umewahusisha pia wakuu wa kanda kutoka TMA na wasimamizi wa vituo vya hali ya hewa-kilimo vinavyoendeshwa na Mamlaka vilivyopo nchini,washiriki watapata fursa ya kujadili na kutolea maamuzi maoni ya wadau wa sekta ya kilimo, nishati, maji, afya na habari na pia kujipanga katika kuwafikia wadau wengine.

IMETOLEWA NA MONICA MUTONI, OFISI YA UHUSIANO TMA





Friday, April 17, 2015

TRAINING AND EMPLOYMENT OPPORTUNITIES


The Director General of the Tanzania Meteorological Agency wishes to re-announce availability of training opportunities for Meteorological Technicians within the Agency. This announcement was earlier made on 12 December 2014. For those who have already applied are not supposed to re-apply.
Qualifications:
  1.  Form six leavers with two principal passes in mathematics and physics. Passes in chemistry and geography will be an added advantage.
  2.  Should be not more than 22 years of age by 12 December 2014.
  3.  Women are highly encouraged to apply.

Mode of application:
Applicants are required to pay a non-refundable processing fee of TShs. 10,000 through NMB Bank, A/C Name-Tanzania Meteorological Agency, A/C No. 20101000013.

Duly filled application forms with detailed curriculum vitae, copies of certified academic certificates, three referees, a recent photograph, daytime telephone numbers and bank pay in slip should be mailed to:

Director General,
Tanzania Meteorological Agency,
P.O. Box 3056,
Fax: + 255-22-2460735
Dar es Salaam.
Email:met@meteo.go.tz

Deadline : 22/April/2015

Please note that application forms may be downloaded from the TMA website wwww.meteo.go.tz or obtained from Tanzania Meteorological Agency Headquarters, 3rd  floor,  Ubungo Plaza, Morogoro Road, Dar es Salaam

It should be noted that applications sent without application forms will not be considered and only short listed candidated will be contacted.

Successfully candidates will be required to undergo one year training course at the Agency’s National Meteorological Training Centre, Kigoma. Employment will only be granted after successful completion of the Course.


Tuesday, April 14, 2015

WAFANYAKAZI WA TMA KATIKA USHIRIKI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA LILILOFANYIKA MOROGORO MWAKA HUU




Wajumbe mbalimbali wakisikiliza na kuchangia mada mbalimbali kwenye baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini sambamba na sekretariat
Bw. Geofrid Chikojo akitoa shukrani zake za dhati kwa menejiment na wafanyakazi wenzie baaada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora.

Tuesday, April 7, 2015

ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA AFARIKI DUNIA




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu Dkt. Mohamed Mhita aliyezaliwa tarehe 17 Februari 1946 na kufariki siku ya  Jumatatu tarehe 06 Aprili 2015 katika hospitali ya Agakhan  jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mhita alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa kwa kipindi cha miaka 8 kuanzia 1992 hadi 1999 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia 1999 hadi 2008. Dr. Mhita kwa kushirikiana na uongozi wa iliyokuwa idara Kuu ya Hali ya Hewa alishiriki katika kuishauri Serikali kuhusu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kutoka iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa.
Pamoja na nafasi ya Mkurugenzi Mkuu pia alikuwa Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani kuanzia mwaka 1992 hadi 2008. Alichaguliwa kuwa Mjumbe katika Baraza Kuu la Shirika la Hali ya Hewa Dunia kuanzia mwaka 1995 hadi 2007. Alichaguliwa  kushika nafasi ya Rais wa Jumuiya ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika (RA 1)  kuanzia mwaka 1998 hadi 2007. Dkt Mhita alikuwa Rais wa ‘Tanzania Meteorological Society’ sambamba na nafasi nyingine nyingi mbalimbali alizoshika ndani na nje ya nchi.
Akielezea baadhi ya mambo makubwa yatakayomfanya Dkt. Mhita aendelee kukumbukwa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi alisema ‘Dkt. Mhita atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sayansi ya hali ya hewa hapa nchini, katika Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla hususani katika ushiriki wake wa kuianzisha Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kwa kuandaa dira (vision) na dhamira (mission) ya Mamlaka kwa kipindi cha miaka kumi na tano (15) kuanzia mwaka 2000 hadi 2015’.  
Dkt. Mohamed Mhita ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa zao la chuo kikuu cha Stolkholm, Sweden ambako alitunukiwa shahada ya hali ya hewa (BSc. Met) mwaka 1977.  Kuanzia mwaka 1981 hadi 1984 alikuwa mafunzoni katika  chuo Kikuu cha Reading, Uingereza ambako alitunikiwa shahada ya uzamivu (PhD). Hapa nchini alipata mafunzo ya Sekondari katika shule za Tanga na Kamrimjee zote zikiwa mkoani Tanga.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajumuika na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu.
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe.

IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI AFISA MAHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...