Thursday, February 19, 2015

WATUMISHI KUMI WA TMA WAPATA MAFUNZO YA MFUMO WA KIJIOGRAFIA (GIS)



Mkurugenzi  wa Huduma za Utafiti na Matumizi TMA Dkt. Ladislaus Chang'a akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi ambaye alikuwa  mgeni rasmi, ili aweze kuongea na wahitimu wa kozi ya wiki mbili ya mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System -GIS) wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu tarehe 19/02/2015.




Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi akiongea na wahitimu wa kozi ya wiki mbili ya mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System -GIS) wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu tarehe 19/02/2015.


Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo hayo Bi. Noberta Sanga akipokea cheti cha kuhitimu kutoka kwa mgeni rasmi Dkt. Agnes Kijazi.


Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo hayo Bw. Musa Kidato akipokea cheti cha kuhitimu kutoka kwa mgeni rasmi Dkt. Agnes Kijazi.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wakufunzi na wahitimu wa mafunzo ya mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System -GIS) wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu tarehe 19/02/2015.

Mafunzo ya Mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System -GIS) yalifanyika kwa watumishi wapatao kumi kutoka Divisheni ya Utafiti na Matumizi, Divisheni ya Huduma za Ufundi na Divisheni ya Huduma za Utabiri kuanzia tarehe 2 - 19 Februari 2015, Makao Makuu  ya TMA.





No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...