Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi akizungumza na wadau wa sekta mbalimbali na wahariri wa vyombo vya habari ( hawapo pichani) inayohusu utabiri wa mvua za msimu wa Machi-Mei 2015, iliyofanyika Kibaha, Pwani Tarehe 26 Februari 2015
Wadau wa sekta mbalimbaliwadau wa sekta mbalimbali na wahariri wa vyombo vya habari wakimsikiliza mkurugenzi mkuu TMA (hayupo pichani) wakati wa warsha inayohusu utabiri wa mvua za msimu wa Machi-Mei 2015,
iliyofanyika Kibaha, Pwani Tarehe 26 Februari 2015
Wadau wa sekta mbalimbaliwadau wa sekta mbalimbali na wahariri wa vyombo
vya habari katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu TMA wakati wa
warsha inayohusu utabiri wa mvua za msimu wa Machi-Mei 2015,
iliyofanyika Kibaha, Pwani Tarehe 26 Februari 2015
Thursday, February 26, 2015
Thursday, February 19, 2015
WATUMISHI KUMI WA TMA WAPATA MAFUNZO YA MFUMO WA KIJIOGRAFIA (GIS)
Mkurugenzi wa Huduma za Utafiti na Matumizi TMA Dkt. Ladislaus Chang'a akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi ambaye alikuwa mgeni rasmi, ili aweze kuongea na wahitimu wa kozi ya
wiki mbili ya mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System
-GIS) wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu tarehe 19/02/2015.
Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi akiongea na wahitimu wa kozi ya wiki mbili ya mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System -GIS) wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu tarehe 19/02/2015.
Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo hayo Bi. Noberta Sanga akipokea cheti cha kuhitimu kutoka kwa mgeni rasmi Dkt. Agnes Kijazi.
Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo hayo Bw. Musa Kidato akipokea cheti cha kuhitimu kutoka kwa mgeni rasmi Dkt. Agnes Kijazi.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wakufunzi na wahitimu wa mafunzo ya mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System -GIS) wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu tarehe 19/02/2015.
Mafunzo ya Mfumo wa Kijiografia (Geographical Information System -GIS) yalifanyika kwa watumishi wapatao kumi kutoka Divisheni ya Utafiti na Matumizi, Divisheni ya Huduma za Ufundi na Divisheni ya Huduma za Utabiri kuanzia tarehe 2 - 19 Februari 2015, Makao Makuu ya TMA.
Sunday, February 15, 2015
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WANAOSIMAMIA HUDUMA ZA HALI YA HEWA AFRIKA (AMCOMET)
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi sambamba na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dkt. Pascal Waniha katika ushiriki wa mkutano huo
Viongozi wa Mamlaka za Hali ya Hewa Afrika katika picha ya pamoja ambapo walikutana kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na changamoto kabla ya mkutano huo
AMCOMET (African Ministerial Committee for Meteorology) ni Kamisheni ya
Mawaziri wanaosimamia huduma za hali ya Hewa Umoja wa Afrika mwaka huu umefanyika katik visiwa vya Cape Verde.Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tibeza.
Kabla ya Mkutano huo Mkutano huo, Viongozi wa Mamlaka za Hali ya Hewa
Afrika walikutana katika mkutano wao kujadili masuala mbalimbali ya
maendeleo na changamoto katika Regional one meeting RA-1 na Technical
Meeting ya AMCOMET
Tuesday, February 10, 2015
SHULE YA JESHI LA WANAMAJI-KIGAMBONI YATEMBELEA OFISI ZA HALI YA HEWA JNIA
Shule ya Kijeshi ya Wanamaji Kigamboni watembelea ofisi za JNIA kwa ajili ya mafunzo. Pichani ni mkuu wa shule hiyo akikabidhi zawadi ya fulana kwa Kaimu Meneja wa Usafiri wa Anga na Maji Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ndugu John Mayunga. Pembeni ni ofisa wa zamu(Duty Forecaster) ndugu Maria Cathbert
Thursday, February 5, 2015
VIONGOZI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA TMA KWENYE MAONESHO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA CHUO CHA USAFIRISHAJI (NIT)
Washiriki wa TMA katika banda la Mamlaka kwenye maadhimisho ya Miaka 40 ya Chuo cha Usafirishaji Bw. Joseph Aliba na Bi.Monica Mutoni wakisikiliza maoni toka kwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Meja Jenerali Joseph Kapwani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Bi. Monica Mwamnyange akiongea na wanachi walifurika katika banda la TMA kuhusu umuhimu wa taarifa zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini
Mkurugenzi Mkuu TMA akifanya mahojiano na vyomba vya habari kwenye banda la TMA katika ushiriki wa maonesho ya miaka 40 ya Chuo cha Usafirishaji(NIT)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Bw. Charles Chacha akisaini kitambu cha wageni alipotembelea banda la TMA
Mkuu wa Chuo cha NIT akisaini kitambu cha wageni alipotembelea banda la TMA
Bw.
John Mayunga akitoa elimu kwa baadhi ya wageni waliotembelea Banda la TMA
Wageni mbalimbali wakitembelea mabanda kupata elimu
Baadhi ya wanachuo wakipata elimu kutoka kwa maafisa wa TMA Bi.Monica Mutoni (Juu) na Bw. Muhidin Mawazo (chini)Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Kijazi akipata maelezo kutoka kwa afisa wa kampuni ya Scania jinsi kampuni ya Scania inavyotoa magari ya kisasa mojawapo ni kuhakikisha dereva aliyetumia kilevi hawezi kuwasha gari wakati alipotembelea baadhi ya mabanda ya taasisi zilizoshiriki katika maonesho hayo.
Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Kijazi akipata maelezo kutoka Mkurugenzi na Mkufuzi wa Chuo cha Marubani (Tanzania Pilot Training Centre) kilichopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa jinsi gani chuo hicho kinatumia taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya mafunzo wakati alipotembelea baadhi ya mabanda ya taasisi zilizoshiriki katika maonesho hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
Dar es Salaam, 22 /0 8 /202 4 ; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za VULI 202 4 kwa maeneo yanayopat...