Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa kidigital wa ukusanyaji, uandaaji na utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) na mfumo wa usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS) kutoka katika vituo 28 vya Mamlaka ya Hali ya Hewa vya uangazi wa hali ya hewa vinavyo pima hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Madhumuni ya warsha hii ya
mafunzo ni kujifunza kuongeza ubora wa uangazi wa hali ya hewa kwa njia za teknolojia
ya kisasa kabisa. Aidha, mafunzo haya yanalenga katika maandalizi ya kuanza
kutumika kwa teknolojia hii katika vituo vyote nchini.
Mifumo hii imetengenezwa na wataalamu wetu wa Mamlaka ya
Hali ya Hewa.
Mifumo hiyo ni:
1.
Mfumo wa kidigitali wa Ukusanyaji, Uandaaji na Utumaji wa taarifa za uangazi wa
hali ya hewa (Digital Meteorological Observatory (DMO)) na
2. Mfumo wa Usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa Usafiri
wa Anga (Meteorological Aviation Information System (MAIS)).
Mifumo hii itapunguza gharama za uendeshaji zinazotokana na utumiaji wa karatasi na kuweka kumbu kumbu, kuboresha mfumo wa mawasiliano
ndani na nje ya nchi kwa maana ya ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za hali
ya hewa kutokana na mahitaji na viwango vya Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(World Meteorological Organization).
Hali
kadhalika, teknolojia hii inarahisisha ufuatiliaji
wa utendaji kazi kwa watoa huduma na kuwawezesha wadau kutoa maoni ya huduma za
hali ya hewa kwa urahisi na haraka zaidi kupitia mifumo hiyo.
No comments:
Post a Comment