Dondoo muhimu kwa ufupi:
Taarifa hii inatoa
tathmini ya mvua za masika (Machi - Mei) 2014 na mwelekeo wa mifumo ya hali ya
hewa na mvua kwa kipindi cha mwezi Oktoba
hadi Disemba, 2014(Vuli).
1.
Mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Oktoba-Disemba,
2014 Vuli unaonyesha kuwa;
·
Hali ya mvua inatarajiwa
kuwa ya kuridhisha katika maeneo mengi
ya nchi
hata hivyo mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi hususan
mkoa wa Ruvuma.
·
Msimu huu mvua
zinatarajiwa kuanza mapema mwezi Septemba katika maeneo ya ziwa Viktoria,
nyanda za juu kaskazini mashariki na pwani ya kasikazini
2. Athari na Ushauri
·
Mvua
za kutosha zinatarajiwa kwa shughuli za kilimo katika maeneo mengi ya nchi.
·
Vina
vya maji katika mito na mabwawa vinatarajiwa kuongezeka katika maeneo mengi ya
nchi.
·
Maji yatumike kwa
uangalifu na kuzingatia taratibu za uvunaji, uhifadhi na matumizi endelevu ya
rasilimali maji
·
Matukio ya migogoro
inayosababishwa na mifugo, wanyamapori na shughuli za binadamu na kilimo
hayatarajiwi kujitokeza kwa kiasi kikubwa.
·
Vipindi
vya mvua kubwa vinaweza kuongeza matukio ya mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu.
·
Milipuko
ya magonjwa yanayosababishwa na kutuama
kwa maji na utiririshaji wa majitaka usiodhibitiwa inaweza kujitokeza.
·
Hatua
stahiki katika utunzaji wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama, na
usambazaji wa madawa, maji na chakula ikiwa ni hatua za kujiandaa na
kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea
Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania