Tuesday, June 21, 2016

TAARIFA KWA WAFANYAKAZI WA MAKAO MAKUU, JNIA NA BANDARINI.
YAH: KUSIKILIZA KERO NA KUPOKEA MAONI MBALIMBALI YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI.
Mkurugenzi Mkuu ameandaa siku ya Jumatano saa 7 mchana Tarehe 22 Juni 2016 ili kusikiliza matatizo sambamba na kupokea maoni mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini. Kazi hii itatolewa katika ukumbi wa Mikutano, ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza-Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kazi hii ni utekelezaji wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini kwa mwaka 2016. 
IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO- MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

1 comment:

  1. Kwa ambao hawataweza kufika,wanaweza kufikisha kero/malalamiko/matatizo/maoni yao kwa njia ipi,,????

    ReplyDelete