Friday, June 27, 2025

MKUU WA MAKAPTENI ZANZIBAR AELEZEA MIPANGO YA SAFARI INAVYOTEGEMEA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.

 





Zanzibar, Tarehe 25 Juni 2025:

Mkuu wa Makapteni Zanzibar, Kapteni Kadadi Hassan Shea, ameelezea namna taarifa za hali ya hewa zinavyowasaidia katika kupanga safari zao baharini na kuepukana na hasara zinazoweza kujitokeza.

Alizungumza hayo kupitia vyombo vya habari alipokuwa ametembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) lililokuwa katika maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar kuanzia Tarehe 22 hadi 25 Juni 2025.

"Taarifa za hali ya hewa zinatusaidia sana katika kufanya mipango ya safari zetu baharini ili kuepusha au kupunguza hasara zinazoweza kujitokeza, mfano kukiwa na utabiri wa uwepo wa upepo mkali huwa tunajipanga kwa kuchukua mizigo kidogo katika kukabiliana nao, na kama kuna utabiri wa uwepo wa mvua tunachukua maamuzi ya kupakia mizigo, kama vile saruji, kwenye makontena," alielezea Kapteni Shea.

Kaptain shea aliongezea kuwa maonesho haya yanawapa fursa Mabaharia kukutana na kufahamiana na taasisi mbalimbali ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuihudumia jamii kwa usalama na faida zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TMA Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Masoud Makame Faki, alisema ushiriki wa Mamlaka katika maonesho hayo yanajielezea kupitia kauli mbiu yake inayosema "Bahari Yetu, Wajibu Wetu na Fursa Yetu," ambapo kupitia kipengele cha wajibu wetu TMA inawajibika katika kuelezea namna huduma za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia katika kuokoa maisha ya mabaharia, wasafiri na mali kwa ujumla.

Monday, June 23, 2025

TMA YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025.

 


Dodoma, tarehe 18 Juni 2025.

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepata fursa ya kushiriki katika maonesho ya kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2025.

 

Kupitia maonesho hayo wageni kutoka sekta mbalimbali nchini wameendelea kutembelea banda la TMA ikiwemo Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ili kujifunza masuala mbalimbali yalioandaliwa katika utoaji elimu juu ya huduma zitolewazo na TMA kwa manufaa ya jamii na maendeleo ya Taifa,

 

Kaulimbiu ya maonesho hayo ni “Kujenga Mifumo Thabiti ya Utoaji Huduma kwa Maendeleo Endelevu”.

 

Monday, June 2, 2025

TMA YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA USHIRIKISHWAJI WA WADAU KATIKA KUONGEZA UELEWA WA MATUMIZI SAHIHI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA SHERIA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.












Dodoma; Tarehe 30 Mei, 2025;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepongezwa na kuhimizwa kuendeleza ushirikiano na wadau wa sektambalimbali za kiuchumi na Kijamii ili kuongeza uelewa wamatumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa pamoja na ufanisikatika  uzingatiaji wa sheria Namba 2 ya mwaka 2019 ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania.

 

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Hali yahewa Tanzania(NMTC) Dkt, Emmanuel Mpeta KatikaUfunguzi wa warsha ya uelewa wa huduma  za hali ya hewazinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwawadau kuitoka sekta mbalimbali nchiniwakiwemoWanahabariMafunzo haya yalifanyika kuanzia Tarehe 27 – 30, Mei 2025  kwenye ukumbi wa Royal village jijiniDodoma.

 

Nawapongeza TMA kwa kuendelea kuwashirikisha wadauwa sekta mbalimbali  kw lengo la kuimarisha matumizi yataarifa ya za hali ya hewa katika shughuli za kijamii nakiuchumiWarsha hii ni fursa muhimu ya kuboresha hudumaza hali ya hewa na kuimarisha matumizi sahihi ya huduma zahali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania, ikiwemo uzingatiaji wa Sheria ya Mamlaka ya Haliya Hewa Na.2 ya 2019 katika shughuli zinazotumia au zinazotakiwa kutumia huduma za hali ya hewa nchiniWarshahii pia ni fursa ya kujenga na kuimarisha uelewa kuhusiana nachangamoto na fursa za mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianchi.” alisema DktMpeta

 

Dkt Mpeta alisisitiza pia umuhimu wa wadau wote kuzingatiasheria Na 2 ya Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania katikashughuli zao za kila siku za kiuchumi na kijamii. “Utekelezajiwa sheria ya Mamlaka unaambatana na jukumu la kusimamiahuduma za hali ya hewa pamoja na udhibiti  wa shughuli zahali ya hewa hapa nchiniMkutano huu ni muhimu katikakuwajengea wadau uelewa wa nini wanapaswa kufanya kwamujibu wa Sheria”.

 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Mabadiliko yaTabianchi DktLadislaus Chang’a aliwashukuru wafadhili waMradi wa  “WISER” na washirika wengine kwa kuendeleakushirikiana na TMA katika kuimarisha huduma za hali yahewa.

AidhaDktChang’a alisisitiza umuhimu wa  kuzingatiamatumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa katika kufanyamaamuzi stahiki wakati woteVilevile aliendelea kuvishukuruvyombo vya habari kwa kuendelea kuwa kiungo cha kutoahabari sahihi za hali ya hewa kwa jamii.

 

Warsha hii imehusisha wadau kutoka sekta mbalimbali zakiuchumi na kijamii nchini kama vile nishatikilimomajihabarimaafaSerikali za Mitaa pamoja na Sekta binafsiMamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaendelea na  juhudi zakuhakikisha jamii inapata uelewa mpana wa taarifa za hali yahewa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa matumizi ya taarifa hizi kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...