Dar es Salaam; Tarehe 02 Novemba, 2022;
Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa ametoa wito kwa wananchi kufuatilia taarifa za hali za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Amesema matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa yainasaidia kutambua hali ikoje katika siku zijazo na hivyo kusaidia kupanga shughuli mbalimbali kwa kushirikiana na wataalam kutoka sekta husika.
“Natoa wito kwa watanzania kutumia taarifa sahihi kutoka TMA ili kuweza kutambua hali ikoje katika shughuli zetu kwa kushirikiana na wataalamu kutoka sekta husika”. Alisema Msigwa wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya TMA kwa mwaka wa fedha 2021/22 na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2022/23, katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Dodoma.
Awali wakati akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, Dkt. Hamza Kabelwa alisema katika kipindi husika, TMA imefanikiwa kutekeleza miradi ya rada, vifaa na miundo mbinu ya hali ya hewa ambapo hatua zilizofikiwa ni asilimia 90 ya utengenezaji wa mtambo wa rada mbili za Mbeya na Kigoma ambapo malipo ya asilimia 90 yamefanyika pamoja mitambo miwiili ya kupima hali ya hewa inayohamishika na ununuzi wa kompyuta maalum ‘cluster computer ilinunuliwa.
“Aidha, Mamlaka ilizinduwa mfumo mpya wa uangazi wa hali ya hewa ya anga za juu katika kituo cha kupima hali ya hewa ya anga ya juu kilichopo JNIA, Mamlaka iliendelea na jukumu lake la kutoa utabiri kwa usahihi, kwa mfano utabiri wa mvua za msimu ulioanza Novemba 2021 hadi Aprili 2022 ulikuwa una usahihi wa asilimia 93.8 ukiwa juu ya kiwango cha usahihi kinachokubalika kimataifa”.
Akielezea matarajio katika mwaka wa fedha 2022/23, Dkt. Kabelwa alisema, matarajio yaliyopo ni pamoja na kupanua wigo wa utoaji wa elimu kwa wananchi na wadau juu ya umuhimu wa huduma za hali ya hewa,kuimariasha uangazi wa hali ya hewa katika Bahari na Maziwa makuu, kuedelea na utekelezaji wa sheria Na. 2 ya mwaka 2019 na kanuni zake pamoja kuboresha miundo mbinu ya Chuo cha taifa cha Hali ya Hewa.
No comments:
Post a Comment