Dondoo
muhimu za mwezi Novemba, 2016
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mifumo ya
hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2016 na mwelekeo wa viashiria vya mifumo ya hali
ya hewa pamoja na mvua katika kipindi cha mwezi Novemba, 2016.
- Mwelekeo wa mvua za Vuli, 2016 kwa kipindi cha mwezi Novemba, 2016:
Hali ya
upungufu wa mvua inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi katika kipindi cha
mwezi Novemba, 2016.
- Maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini mashariki pamoja na maeneo ya mkoa wa Tabora mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Novemba,2016.