Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania TMA, wizara
ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto na Taasis ya kusimamia Anga
na Bahari kutoka Marekani (NOAA) wameandaa warsha ya siku tatu kuanzia tarehe
10 mpaka 12 Agosti 2016 yenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali katika
sekta ya hali ya hewa na sekta ya afya
ili kujadili changamoto zitokanazo na hali ya hewa zinazokabili sekkta ya afya.
Akifungua warsha hiyo katika ukumbi wa Ramada kwa
niaba ya mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA ambaye pia ni mjumbe wa Bodi
Prof. Msola alizungumzia umuhimu wa kukaa na wadau husika ili kuweza kusikia
mahitaji yao kwa maendeleo ya nchi na ulimwenguni kwa ujumla, ikizingatiwa
kwamba ulimwenguni kote kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa
hivyo ni muhimu kutambua maeneo mahususi ya kutiliwa mkazo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka TMA Dkt. Ladislaus Changa
alishukuru kwa niaba ya TMA na Serikali ya Tanzania kwa kupata hiyo nafasi ya kukutana na wadau
kupitia ufadhili wa NOAA na kuahidi ushirikiano mkubwa kati ya TMA na Wizara ya
afya,Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto sambamba na taasisi zingine
zinazoshughulikia masuala ya afya, ushirikiano huo utasaidia uboreshaji wa
huduma zitolewazo za hali ya hewa kwa sekta ya afya.
Mwakilishi kutoka NOAA Dkt.Wassila Thaw alielezea
umuhimu wa wao kufadhili na kushiriki ni pamoja na kuhakikisha maazimio yote ya
warsha hii yanatafutia ufumbuzi kwa vile moja ya majukumu ya NOAA ni pamoja na
kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinatumika katika sekta za afya kwa matokea
chanya.
Warsha hii imejumuisha wadau kutoka Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya Kilimo na Mifugo, IRI,ICPAC
Kenya,NOAA, IRI, NASA, Chuo Kikuu Chicago kutoka Marekani, Taasisi ya Hali ya
Hewa Ethiopia, Madagascar,Kenya, Uganda,Mozambique, Wizara za Afya Kenya,
Ethiopia, Uganda, WMO, WHO pamoja na
Chuo Kikuu Muhimbili.
IMETOLEWA NA MONICA
MUTONI, AFISA UHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment