Friday, October 9, 2015

TANZANIA YACHAGULIWA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA TAASISI ZA HALI YA HEWA KUSINI MWA AFRIKA (MASA) KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI. UCHAGUZI HUO ULIFANYIKA WAKATI WA MKUTANO MKUU WA TISA (9) WA UMOJA WA TAASISI ZA HALI YA HEWA ZA KUSINI MWA AFRIKA CAPE TOWN, AFRIKA KUSINI, 30 SEPTEMBA – 2 OCKTOBA 2015 “Ninth Meteorological Association of Southern Africa (MASA) Annual General Meeting (AGM IX)”

Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania akiwa na wakuu wa Taasisi za hali ya Hewa katika nchi za SADC walipohudhuria mkutano wa MASA na SCOM jijini Cape Town nchini Afrika Kusini

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi na Meneja wa Mahusiano ya Kimataifa, Ndugu Wilbert Timiza walishiriki katika Mkutano Mkuu wa Tisa (9) wa Umoja wa Taasisi za Hali ya Hewa za Kusini mwa Afrika (“Ninth Meteorological Association of Southern Africa (MASA) Annual General Meeting (AGM IX)”) uliofanyika Cape Town, Afrika Kusini kuanzia tarehe 30 September hadi 2 Oktoba 2015. 

Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulijadili masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano katika nyanja ya hali hewa kwa taasis za hali ya hewa katika nchi wanachama wa SADC na kupitisha Mpango Mkakati wa utekelezaji wa masuala ya hali ya hewa kanda ya SADC (MASA Strategic Plan). Mkutano huo pia umejadili utekelezaji wa programu mbali mbali zinazotekelezwa na nchi wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)  kama vile “Global Framework for Climate Services (GFCS)”, “WMO Integrated Global Observing System and Information System (WIGOS/WIS), utoaji wa tahadhari za mapema ili kukabiliana na maafa “High impact services for disaster risk reduction”, Uboreshaji wa huduma za usalama na usafiri wa anga “Aviation meteorological services”.

Aidha, Mkutano huo ulichagua Mwenyekiti mpya wa MASA pamoja na Bodi Mpya ya MASA baada ya Uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake. Dkt Agnes Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ambaye alikuwa mjumbe katika Bodi ya MASA iliyomaliza muda wake alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa MASA akiiwakilisha Tanzania ambapo Namibia ilichaguliwa kuwa Mwenyekiti. Tanzania pia ilichaguliwa kuongoza kamati ya Uongozi na uendelezaji wa Rasilimali (Institutional Management and Capacity Development Committee), kuwa katika vikosi kazi mbalimbali vya MASA ambapo watumishi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania watashiriki kama wajumbe.

Mkutano huo wa MASA ulifuatiwa na Mkutano wa ‘SADC Committee of Meteorology (SCOM)’ ambao ulihudhuriwa na wakuu hao wa taasisi za hali ya Hewa katika nchi za SADC na kusimamiwa na SADC Secretariat.
IMETOLEWA NA:
MONICA MUTONI
AFISA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...