Wednesday, October 15, 2014

TMA YAJUMUIKA NA MATAIFA 12 YALIYOKUTANA DAR KUZINDUA CIRDA PAMOJA NA KUBADILISHANA UTAALAMU WA NAMNA YA KUHUDUMIA WANANCHI KUPITIA TAARUFA ZITOLEWAZO NA MAMLAKA ZA HALI YA HEWA

Meneja wa mradi wa CIRDA kutoka UNDP, Bonizella Biagini akizungumza wakati akitambulisha maofisa waliokuwepo katika uzinduzi wa warsha ya siku tatu ya kimataifa ya ukusanyaji na matumizi ya taarifa ya hali ya hewa kwa nchi 12 duniani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Mipango ya maendeleo duniani (UNDP) Phillippe Poinsot, Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi.

Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi akifungua mafunzo hayo ya siku tatu kwa wataalamu wa hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi na wanaojihuisha na majanga kutoka nchi 12 ikiwemo Tanzania katika mpango wa CIRDA.
 Dkt. Pascal F.Waniha mwakilishi wa mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa akitoa mada wakati warsha hiyo.
 Mkurugenzi mkazi wa UNDP Philippe Poinsot akihutubia katika warsha hiyo.
 Mmoja wa watoa mada Jeremy Usher kutoka CIRDA akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa takwimu na uangaliaji wa mifumo katika dunia inayokabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi.
 Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza mada kwa makini.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ndugu Richard Muyungi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.


CIRDA ni mpango wa kiutafiti wa mfumo wa hali ya hewa na mabadiliko yake unaozingatia upatikanaji wa data za hali ya hewa na kuzifikisha maeneo husika kwa matumizi na kwa wakati.
 
Mradi huo umelenga kuhakikisha wakulima, watunga sera na sekta binafsi wanafanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa za hali ya hewa kutokana na mabadiliko makubwa yaliyopo sasa.
 
 Mataifa 11 ikiwemo Tanzania yanakutana jijini Dar kwa mafunzo ya siku tatu yanayohusu utengenezaji wa mifumo bora ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa,uchakataji wake na matumizi ya taarifa hizo kwa wananchi wa kawaida na watunga sera ili kuwa na uhakika na Mipango ya maendeleo.
 
Mataifa hayo ni yale yalioyopo katika mradi wa Multi Country Support Programme to Strengthen Climate Information Systems in Africa (CIRDA).
Nchi zinazohusika katika mpango huu pamoja na wenyeji Tanzania ni Benin, Burkina Faso, Ethiopia, the Gambia Liberia, Malawi, Sierra Leone, Sao Tome and Principe,Uganda na Zambia.
 
 Warsha hiyo inayofanyika katika hoteli ya Whitesands iliyopo Dar es Salaam imelenga kutoa na kubadilishana utaalamu wa namna ya kuhudumia wananchi kupitia data zinazotolewa na Mamlaka za Hali ya Hewa na taasisi za kukabiliana na majanga.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...