Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi akifungua mafunzo hayo ya siku tatu kwa wataalamu wa hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi na wanaojihuisha na majanga kutoka nchi 12 ikiwemo Tanzania katika mpango wa CIRDA.
Dkt. Pascal F.Waniha mwakilishi wa mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa akitoa mada wakati warsha hiyo.
Mkurugenzi mkazi wa UNDP Philippe Poinsot akihutubia katika warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza mada kwa makini.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ndugu Richard Muyungi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
CIRDA
ni mpango wa kiutafiti wa mfumo wa hali ya hewa na mabadiliko yake
unaozingatia upatikanaji wa data za hali ya hewa na kuzifikisha maeneo
husika kwa matumizi na kwa wakati.
Mradi
huo umelenga kuhakikisha wakulima, watunga sera na sekta binafsi
wanafanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa za hali ya hewa kutokana na
mabadiliko makubwa yaliyopo sasa.
Mataifa
11 ikiwemo Tanzania yanakutana jijini Dar kwa mafunzo ya siku tatu
yanayohusu utengenezaji wa mifumo bora ya upatikanaji wa taarifa za hali
ya hewa,uchakataji wake na matumizi ya taarifa hizo kwa wananchi wa
kawaida na watunga sera ili kuwa na uhakika na Mipango ya maendeleo.
Mataifa
hayo ni yale yalioyopo katika mradi wa Multi Country Support Programme
to Strengthen Climate Information Systems in Africa (CIRDA).
Nchi
zinazohusika katika mpango huu pamoja na wenyeji Tanzania ni Benin,
Burkina Faso, Ethiopia, the Gambia Liberia, Malawi, Sierra Leone, Sao
Tome and Principe,Uganda na Zambia.
Warsha
hiyo inayofanyika katika hoteli ya Whitesands iliyopo Dar es Salaam imelenga kutoa na
kubadilishana utaalamu wa namna ya kuhudumia wananchi kupitia data
zinazotolewa na Mamlaka za Hali ya Hewa na taasisi za kukabiliana na
majanga.