Monday, September 22, 2014

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI DR. CHARLES TIZEBA AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA TAASIS ZA HALI YA HEWA KUTOKA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SADC)

Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akihutubia wakuu wa taasis za hali ya hewa kutoka kusini mwa Afrika (SADC) katika mkutano wao uliofanyika mjini Arusha katika hoteli ya Palace.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agens Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba kuhutubia wakuu wa taasisi za hali ya hewa Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huu ulihudhuriwa na nchi wanachama wa SADC pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba( wa tatu kutoka kushoto waliokaa), Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi (wa pili kutoka kushoto walikaa) katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa wakuu wa taasisi za hali ya hewa kutoka nchi za Kusini mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment