Friday, November 28, 2025

HALI YA JOTO KALI NCHINI

 


Dar es Salaam, 28 Novemba, 2025:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inapenda kutoa taarifa ya hali la joto katika maeneo mbalimbali nchini. 

Kumekuwepo na ongezeko la Joto katika baadhi ya maeneo hapa nchini hususan yale yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka kwa miezi ya hivi karibuni. Hali hii imesababishwa na kusogea kwa Jua la Utosisambamba na upungufu wa mvua unaojitokeza katika maeneo hayo. Kwa kawaida vipindi vya Jua la Utosi nchini hufikia kilele mwishoni mwa mwezi Novemba wakati Jua la Utosi likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena mwezi Februari wakati Jua la Utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa). Jua la Utosi huambatana na hali ya ongezeko la Joto kwa sababu uso wa Dunia katika eneo tajwa huwa karibu zaidi na Jua kuliko maeneo mengine. 

Katika kipindi cha mwezi Novemba2025 hali ya ongezeko la Joto imeendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, ambapo hadi kufikia tarehe 27 Novemba2025 kituo cha hali ya hewa cha Moshi (Kilimanjaro)kiliripoti kiwango cha juu zaidi cha nyuzi joto 35.7°C mnamo tarehe 21 Novemba, 2025 ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 4.2°C ukilinganisha na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Novemba katika kituo hicho. Kituo cha hali ya hewa cha Ilonga (Morogoro) kiliripoti nyuzi joto 35.5°C mnamo tarehe 20 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 2.7°C). Kituo cha hali ya hewa Morogoro kiliripoti nyuzi joto 34.5°C mnamo tarehe 26 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 2.3°C). Kituo cha Ibadakuli (Shinyanga) kiliripoti nyuzi joto 33.6°C mnamo tarehe 14 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 2.2°C), na Dar es salaam nyuzi joto 33.2 °Cmnamo tarehe 19 na 21 Novemba (ongezeko la nyuzi joto 1.6°C).

Aidha, ongezeko la unyevu angani (Relative humidity) katika kipindi hiki linalosababishwa na mvuke wa Bahari hususan katika maeneo ya ukanda wa pwani na maeneo jirani limechangia pia mwili kuhisi joto zaidi ya viwango vinavyoripotiwa.

Hata hivyo, katika kipindi cha mwezi Desemba, 2025vipindi vya mvua vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi nchini. Hali hii inatarajiwa kusababisha kupungua kwa Joto katika baadhi ya maeneo hususan yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Kwa taarifa hii wananchi wanashauriwa kuendelea kuzingatia taarifa na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania sambamba na kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazotokana na hali mbaya ya hewa.

Monday, November 17, 2025

TANZANIA YAIMARISHA UWEZO WA BURUNDI KATIKA USIMAMIZI WA UBORA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA



30 Oktoba, 2025: Bunjumbura, Burundi

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ikishirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Taasisi ya Hali ya Hewa ya Burundi (IGEBU), ilifanikiwa kufanya mafunzo ya kujenga uwezo wa Mfumo wa Udhibiti wa Ubora (QMS) kwa wafanyakazi zaidi ya arobaini (40) wa IGEBU, mjini Bujumbura, Burundi, kuanzia tarehe 13 hadi 30 Oktoba 2025. Mafunzo hayo yalitolewa na wataalamu wa TMA kupitia mfumo wa ushirikiano wa kimataifa wa huduma za hali ya hewa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kupitia mpango wa WMO wa Athari za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari ya Mapema Afrika Mashariki (CREWS), mafunzo hayo yalilenga kujenga uwezo wa kitaasisi wa IGEBU ili kuoanisha mifumo yake kwa kiwango cha udhibiti ubora cha ISO 9001:2015. Wataalamu wa QMS kutoka TMA, walitoa mafunzo endelevu kwa wafanyakazi wa IGEBU, kuwaongoza kupitia  ukaguzi wa ndani na mipango ya usimamizi.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo katika ukumbi wa Chandelier, Bujumbura, Burundi, Mkurugenzi wa Ofisi ya WMO Kanda ya Afrika, Dkt. Agnes Kijazi alipongeza dhamira ya IGEBU na mchango wa Tanzania katika kujenga uwezo wa kikanda.

"Dhamira hii ni ushuhuda wa kile kinachoweza kupatikana kupitia ushirikiano kwa kuwekeza katika mifumo bora, kuimarisha imani katika huduma za hali ya hewa, msingi wa ustahimilivu na maendeleo endelevu." Alisema, Dkt Kijazi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Taasisi ya Hali ya Hewa ya Burundi (IGEBU), Bw. Deogratius Babonwanayo, alitoa shukrani kwa mafunzo yaliyotolewa na kuthibitisha dhamira ya IGEBU ya kuelekea kwenye Mfumo wa Udhibiti Ubora (QMS). 

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Mabadiliko ya Sayansi ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a alishiriki kwa njia ya mtandao, akithibitisha kuendelea kujitolea kwa TMA katika maendeleo ya kikanda kupitia ushirikiano na kubadilishana ujuzi.

Mafunzo ya QMS yalilenga kuimarisha mifumo ya ndani ya IGEBU na kuimarisha mshikamano wa kikanda katika kutoa huduma za hali ya hewa zenye ubora. Juhudi hizo zinaletwa na msukumo wa kimataifa wa WMO ili kuhakikisha nchi zote zinaweza kutoa taarifa za hali ya hewa zenye ubora kwa wakati, zitakazoaminika na zinazoweza kutekelezeka kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi katika shughuli zote za kijamii na kiuchumi na kulinda maisha ya watu na mali zao.

Friday, November 14, 2025

Tanzania Strengthens Burundi’s Path Toward Quality Management in Meteorological Services: Tanzania–Burundi Partnership in Action

 













30 October 2025, Bujumbura, Burundi

The Tanzania Meteorological Authority (TMA), in close collaboration with the World Meteorological Organization (WMO) and the Institut Géographique du Burundi (IGEBU), successfully concluded a Quality Management System (QMS) capacity-building mission in Bujumbura, Burundi, from 13 to 30 October 2025. This technical assistance, delivered by TMA experts through a South–South cooperation framework, reflects Tanzania’s leadership in advancing operational excellence in meteorological services across East Africa.

Implemented through the WMO Climate Risk and Early Warning Systems (CREWS) East Africa initiative, the mission focused on building the institutional and human capacity of IGEBU to align its processes with the ISO 9001:2015 QMS standard. The TMA delegation, composed of QMS experts Mr. Geofrid Chikojo and Mr. Danford Nyenyema, provided sustained on-the-ground mentorship to IGEBU staff, guiding them through training sessions, internal audit simulations, and management planning.

The closing ceremony, held at Le Chandelier in Bujumbura, was graced by Dr. Agnes Kijazi, Director of the WMO Regional Office for Africa, who praised both IGEBU’s commitment and Tanzania’s contribution to regional capacity-building.

She remarked, “This mission is a powerful testament to what can be achieved through South–South collaboration. By investing in quality systems, we are strengthening trust in our climate and weather services, the cornerstone of resilience and sustainable development.”

In her address, Dr. Kijazi also acknowledged the instrumental role of TMA in supporting peer institutions in the region, noting that such technical missions promote long-term sustainability, standardization, and shared excellence across African National Meteorological and Hydrological Services (NMHSs).

The event was also attended by the Permanent Representative of Burundi with WMO Mr Deogratius Babonwanayo, who expressed appreciation for the support received and reaffirmed IGEBU’s commitment to moving toward QMS certification. The Permanent Representative of Tanzania with WMO and IPCC Vice Chair, Dr. Ladislaus Chang’a participated virtually, reaffirming TMA’s dedication to regional advancement through cooperation and knowledge exchange.

Throughout the mission, IGEBU established a dedicated internal audit team, conducted its first management review meeting, and mobilized over 40 staff members in practical training activities. A comprehensive internal audit simulation was successfully implemented, and a tailored roadmap for ISO 9001:2015 certification was developed.

This QMS mission not only strengthened IGEBU’s internal systems but also reinforced regional solidarity in delivering high-quality, user-oriented meteorological and climate services. The effort aligns with WMO’s global push to ensure that all countries can deliver quality, reliable, timely, and actionable weather and climate information and products  for informed decision making in all socio-economic activities and for protection of life and properties amid growing climate risks.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...