Wednesday, July 21, 2021
Saturday, July 10, 2021
NAIBU SPIKA: VYOMBO VYA HABARI TENGENI MUDA WA KUTOSHA KURUSHA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akijionea hindi utabiri wa hali ua hewa kila siku unavyorekodiwa katika studio za TMA kwa ajili ya kuruka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna uchambuzi wa hali ya hewa unavyofanyika kwa njia ya modeli za kimahesabu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna utabiri wa hali ya hewa unavyoandaliwa kuanzia ngazi za awali kutoka kwa Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri, TMA, Bw. Samwel Mbuya wakati alipotembelea ofisi za TMA, Kituo Kikuu cha Utabiri, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo ya namna taarifa za hali ya hewa za muda mrefu zinavyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya kimkakati kutoka kwa Meneja wa Klimatolojia, TMA, Dkt. Hashim Ng'ongolo wakati alipotembelea ofisi za TMA, Makao Makuu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tarehe 09/07/2021.
Dar es Salaam; Tarehe 09 Julai, 2021;
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (MB) ametoa wito kwa vyombo vya habari kutenga muda wa kutosha wa kurusha taarifa za hali ya hewa mara kwa mara ili kusaidia wananchi kuzipata kwa wakati na kuzitumia kwa ufanisi zaidi. Aidha, alieleza kuwa kutokana na muda wa habari ya hali ya hewa kuwa mfupi, taarifa zinatolewa kwa ujumla na kwa ufupi, kitu ambacho kinaweza kuathiri matumizi yake.
“Nitoe wito kwa vyombo vya habari kuangalia namna ambavyo watakuwa wanazitumia taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kuzitoa mara kwa mara ili kutusaidia sisi wananchi kujiandaa na kufanya maamuzi sahihi katika mipango yetu, tuangalie kama vyombo vingine vya habari vya mataifa ya nje, ukifungua kila wakati unaangalia hali ya hewa”Alisema Dkt. Tulia wakati alipotembelea Makao Makuu ya TMA.
Aliendelea kusema kuwa, alichojifunza katika ziara yake fupi katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, ni kuwa taarifa zipo, lakini kwa ajili ya muda mfupi basi Mamlaka inalazimika kuziweka katika huo muda mfupi.
Kwa upande mwingine, alito wito kwa wananchi kuitembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ili kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna taarifa za hali ya hewa zinavyochakatwa kitaalamu hadi kumfikia mtumiaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
Dar es Salaam, 22 /0 8 /202 4 ; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za VULI 202 4 kwa maeneo yanayopat...