Friday, July 31, 2020
Friday, July 24, 2020
Wednesday, July 8, 2020
Wednesday, July 1, 2020
BODI YA TMA YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA RADA YA HALI YA HEWA MTWARA.
Wajumbe wa Bodi ya TMA katika picha ya pamoja katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara. |
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi, akiwapokea wajumbe wa Bodi ya TMA mara walipowasili katika ofisi za TMA, Kanda ya Kusini ili kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara |
Meneja wa Kanda ya Kusini TMA, ndugu Amasi Daudi akitoa taarifa ya Kanda ya Kusini. |
Msanifu Majengo - TMA, Alfa Buzenzeli akielezea hatua mbalimbali zilizopitiwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara. |
Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kusini TMA, ndugu Amasi Daudi. |
Wajumbe wa Bodi ya TMA, wakikagua baadhi ya vifaa vya Rada za hali ya hewa vilivyokwisha kuwasili hapa nchini katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara. |
Wajumbe wa Bodi ya TMA katika picha ya pamoja walipotembelea ofisi ya TMA, Kanda ya Kusini, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara. |
Kibao kilichopo Barabara Kuu - Mtwara, kinachoelekeza barabara ya mchepuko kuelekea kwenye Rada ya hali ya hewa. |
Meneja wa mipango na ufuatiliaji-TMA, ndugu. Shabani Kidimwa akifafanua jambo wakati wajumbe wa bodi ya TMA walipofika katika eneo la ujenzi wa mradi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara |
Wajumbe wa Bodi ya TMA wakikagua bango lililosimikwa kuutambulisha mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara. |
Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa uzio wa ukuta unaozunguka majengo na eneo itakaposimikwa Rada ya hali ya hewa - Mtwara. |
Wajumbe wa Bodi ya TMA katika picha ya pamoja wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wa TMA na wakandarasi wa mradi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara. |
Mtwara,Tarehe
28/06/2020:
Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya ziara
ya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Rada ya hali ya hewa unaogharimu kiasi
cha zaidi ya Tsh. Bilioni 6, rada hiyo inayotarajiwa kufungwa katika kilima cha
Mbae, Mtwara, ambapo utekelezaji wake umefikia
zaidi ya asilimia 80 na kuleta maendeleo mbalimbali ikiwemo miundombinu
ya barabara, maji na umeme kwa kaya zaidi ya 750 za Mtaa wa Mbae ‘A’.
Akizungumza baada ya kukagua majengo ya
eneo hilo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi kutoka Dar es Salaam alimtaka
mkandarasi ahakikishe anamaliza sehemu iliyobaki kulingana na makubaliano ya mkataba pamoja na kuwa
imetokea changamoto ya COVID 19 iliyopelekea wataalamu wanaotakiwa kuja
kuifunga rada hiyo kutoka Marekani kushindwa kufanya hivyo.
Aidha, aliishukuru Serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili
ya Rada hiyo kwa vile itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mikoa ya Kusini,
huku akiomba uongozi wa mkoa wa Mtwara kuhakikisha eneo la Rada linakuwa salama
wakati wote.
“Ningeomba sana uongozi wa
mkoa wajaribu kuangalia barabara isiharibike, hili ni tatizo ambalo nimeliona
sehemu nyingine, barabara kama hii imetengenezwa baada ya muda unakuta imeharibika
kwa sababu ya kukosa usimamizi wa kutosha kutoka katika uongozi wa eneo
husika”. Alizungumza Dkt. Nyenzi
Kwa upande mwingine, Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya TMA, Prof. Makame Omar Makame kutoka Zanzibar alielezea shukrani zake
kwa serikali kwa vile umuhimu wa rada hiyo ni kwa manufaa ya nchi nzima kwa
vile taarifa zitazopatikana zitasaidia maendeleo ya nchi katika sekta
mbalimbali kama vile usafiri wa baharini, nchi kavu, uvivu, kilimo n.k
“Rada hii ni muhimu kwa mwambao wa bahari
ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba lakini pia katika mwambao wa Dar es Salaam
mpaka kufikia Mtwara, hivyo kumalizika kwake kutatoa fursa ya kupata taarifa
zenye usahihi wa utabiri wa hali ya hewa kwa shughuli mbalimbali”. Aliongezea
Prof. Makame.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
TMA na makamu wa tatu wa rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi
aliishukuru Bodi hiyo kwa kutembelea eneo la Rada na pia aliishukuru Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuendelea
kuboresha huduma za hali ya hewa nchini. Alieleza kuwa, ufungwaji wa rada hiyo
utasaidia wananchi wa mikoa ya kusini kupata taarifa sahihi kwa vile ina uwezo
wa kuona maeneo madogomadogo zaidi na kuweza kutambua aina ya mvua, eneo mvua inaponyesha, kuona matone ya mvua,
vimbunga na hivyo kusaidia kuboresha utabiri kwa ujumla.
“Serikali imekwisha
kulipia rada mbili ambazo zitafungwa Mbeya na Kigoma, hapo utaona katika
mtandao wa rada ukijumuisha Dar es Salaam, Mwanza na hii ya Mtwara utakuwa
umefikia rada tano lakini matarajio yetu ni kuwa na rada saba nchini, tayari
Mamlaka imekwisha kutengewa bajeti katika mwaka wa fedha 2020/21 ya kufunga
rada mbili za Dodoma na Kilimanjaro, hivyo kufikia mwaka ujao wa fedha, Mamlaka
itakuwa imekamilisha idadi ya rada saba zinazohitajika nchini”. Aliongeza Dkt. Kijazi.
Aliendelea kwa kuelezea
vifaa vyote vya rada vimekwishafika na kwamba wanasubiriwa wataalamu kutoka
Marekani ambao wamekwama kutokana na janga la COVID 19, vile vile alieleza kuwa
eneo hilo la ujenzi limejumuisha jengo la mtambo, jengo la wataalamu, jengo la
mlinzi, ukuta na mnara utakaoshika antenna ya rada. Kwa upande wa namna TMA
ilivyojipanga, Dkt. Kijazi alisema tayari waatalam wa ndani wamepatiwa mafunzo
ikiwa na kufanikiwa kufika mpaka kiwandani, hivyo kazi iliyobakia ni kuleta
matokea chanya kwa maendeleo ya nchi.
Ziara ya Bodi hiyo
ilifanikiwa pia kwa kutembelea ofisi ya TMA Kanda-Mtwara na kujionea shughuli
za Ofisi hiyo pamoja na kupata taarifa fupi ya Kanda kutoka kwa Meneja wa Kanda
hiyo Ndugu. Amas Daudi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
06 Septemba 2024, Dar es Salaam: Wahandisi nchini wamekumbushwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa sambamba na kuchangia gharama za upatik...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...