Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akiongea na vyombo vya habari (hawapo pichani) |
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu swali kwa vyombo vya habari (hawapo pichani) |
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Agnes Kijazi akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) |
Baadhi ya wanahabari katika picha |
MAADHIMISHO YA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI
TAREHE 23 MACHI, 2017
Kila mwaka ifikapo tarehe 23 Machi nchi wanachama 190
wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani hujiunga kuadhimisha kuzaliwa kwa Shirika
hilo lililoanzishwa tarehe 23 Machi, 1950 kulingana na kauli mbiu teule. Kauli
mbiu ya mwaka huu ni ’Tuyaelewe mawingu na umuhimu wake’- ”(Understanding
clouds)”.
Katika kuadhimisha Siku
ya Hali ya Hewa Duniani (WMD), Shirika la Hali ya Hewa Duniani limetambua umuhimu wa
kuongeza uelewa wa mawingu ili kujua zaidi mchango wake katika mzunguko wa maji
kati ya nchi kavu, baharini na angan,i na uhusiano wake na hali ya hewa ya muda
mfupi na mrefu. Kama inavyojulikana kuwa mawingu yana umuhimu mkubwa sana
katika mifumo ya hali ya hewa ya dunia na hivyo elimu juu ya tabia ya mawingu
itasaidia katika kutabiri hali ya hewa na kutambua mabadiliko ya tabia nchi kwa
wakati ujao. Wahenga huwa wanasema, Dalili
ya Mvua ni Mawingu.
Kama ilivyo kwa wanachama wengine, Tanzania
inaungana nao kuadhimisha siku hii inayofikia kilele leo tarehe 23 Machi, 2017
kwa kuwakaribisha wananchi wote kutembelea vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona
shughuli zitolewazo na Mamlaka na kujifunza. Aidha, Mamlaka itambelea na kutoa
elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbali mbali nchini kupitia ofisi
zake zilizopo nchi nzima. Kutoa makala za siku hiyo kwenye magazeti, vipindi kwenye radio, televisheni na
mitandao ya kijamii kuhusu elimu juu ya mawingu na sayansi hali ya hewa kwa
ujumla, hii itasaidia kuongeza wigo wa elimu kwa umma hususani mashuleni.
Tunawatakia maadhimisho mema ya Siku ya Hali ya
Hewa Duniani
’Tuyaelewe mawingu na umuhimu wake’
(Understanding Clouds)
Kupata makala za Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi ingia humu http://www.meteo.go.tz/news/74