Wednesday, January 16, 2019

TMA YASHIRIKI VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE ZA MIUNDOMBINU.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakiwa katika kikao  kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi wakati akiwasilisha mada katika kikao cha Kamati hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi wakati akiwasilisha mada katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Mindombinu katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma, kushoto kwake ni mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Kakoso.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma wakimsikiliza Mwanasheria wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Bw. Emmanuel Ntenga wakati akiwasilisha mada katika kikao cha Kamati hiyo.
Mwanasheria wa Bunge, Ndugu Thomas Shawa akiwapitisha wajumbe wa Kamati ya Miundombinu katika Muswada Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa mwaka 2018 unaotarajiwa kuwasilishwa na Serikali katika Kamati hiyo Januari 16, 2019. Wa kwanza ni mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Kakoso.Kikao hicho cha Kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Chanzo: Michuzi blog


No comments:

Post a Comment