Friday, August 2, 2019

TMA YAENDELEA KUTEKELEZA MAAGIZO YA MAKAMU WA RAIS KWENYE MAONESHO YA NANENANE 2019 KWA KUTOA ELIMU KWA WADAU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika ufunguzi wa maonesho ya nanenane 2019, Simiyu. Kushoto ni waziri wa kilimo Japhet Hasunga na kulia ni Mkuu wa mkoa Simiyu Anthony Mtaka

Elimu ya sayansi ya hali ya hewa ikiendelea kutolewa - Simiyu


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeshiriki katika maonesho ya 27 ya Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Mwakangale mkoani Mbeya, viwanja vya Nanenane Mkoani Morogoro na kitaifa kwa mara ya pili yanafanyika katika viwanja vya nyakabindi mkoani Simiyu, yaliyoenda sambamba na kauli mbiu isemayo “ Kilimo, mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa Nchi.
  
Katika ufunguzi wa maonesho hayo tarehe 01 Agosti 2019, Mhe. Samia aliwataka watafiti wote nchini kutoa matokeo ya utafiti kwa walengwa kwa kuwapatia elimu ya kutosha ili waweze kunufaika na tafiti hizo.
“Nitoe rai kwa watafiti wote nchini kutoa matokeo ya tafiti zenu kwa walengwa na kuwapa elimu ya kutosha ili waweze kunufaika ipasavyo” aliongea mama Samia.

Katika kufanikisha rai hiyo ya Makamu wa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, TMA imeanza kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya umuhimu wa kutumia taarifa za hali ya hewa katika kufanya shughuli zao zenye kuleta tija hususani wakulima na wavuvi ambapo zoezi la utoaji wa elimu hiyo linatarajiwa kuendelea mpaka siku ya kilele cha maadhimisho hayo tarehe 08 Agosti 2019.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment