Tuesday, July 23, 2019

WADAU KUTOKA SEKTA ZA UVUVI NA USAFIRISHAJI MKOA WA PWANI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA KUHAKIKISHA JAMII INAELEWA NA KUZITUMIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.















Mkurugenzi wa Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza Kabelwa(katikati mwenye suti nyeupe) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa mafunzo ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta za uvuvi na usafirishaji, tarehe 18 – 20 Julai 2019, Kibaha, Pwani



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, iliandaa warsha ya siku tatu kwa wadau wa sekta za uvuvi na Usafirishaji, iliyofanyika Kibaha, Mkoa wa Pwani, tarehe 18 – 20 Julai 2019, kuwaelimisha juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta zao, kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Weather and Climate Information services for Africa (WISER II)”

Mkurugenzi wa Utabiri wa TMA Dkt. Hamza Kabelwa alikuwa mgeni rasmi katika warsha hiyo. Katika hotuba yake aliwataka washiriki kutoa ushirikiano katika kuchangia mada mbalimbali zitakazowasilishwa kwao, ili kwa pamoja kutoa huduma bora za hali ya hewa kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu na kusaidia kuokoa maisha ya watu na mali zao sambamba na kuongeza kipato katika shughuli zao za kila siku
“Mtakapofikia mwisho wa warsha hii naamini ninyi mtakuwa mabalozi wazuri na mtashirikiana na TMA kuhakikisha elimu mliyoipata hapa inasambaa  na kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia walengwa na kuzitumia ipasavyo” aliyasema hayo Dkt. Hamza Kabelwa.

Aidha, washiriki waliishukuru TMA kwa kuandaa mafunzo hayo kwa kuwachagua wao kama wawakilishi wa wenzao, hivyo waliahidi elimu waliyoipata wataifanyia kazi na kuisambaza katika sekta zao hususani jamii inayowazunguka.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...