Tuesday, July 30, 2019

TMA YAJUMUIKA NA WADAU WENGINE WA BAHARI KUADHIMISHA WIKI YA BAHARI AFRIKA 2019

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandika akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa wakati wa maadhimisho ya siku ya bahari Afrika  yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ubaharia (DMI), Dar es Salaam, tarehe 24 mpaka 26 Julai 2019
Naibu Waziri wa Uchukuzi-Zanzibar, Mhe. Mohamed Ahmada salum akitoa pongezi zake kwa TMA kwa kazi nzuri inayofanyika ya kutoa tahadhari za hali ya mbaya ya hewa kwa watumiaji wa bahari wakati wa maadhimisho ya siku ya bahari Afrika  yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ubaharia (DMI), Dar es Salaam, tarehe 24 mpaka 26 Julai 2019
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa wakati wa maadhimisho ya siku ya bahari Afrika  yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ubaharia (DMI), Dar es Salaam, tarehe 24 mpaka 26 Julai 2019
Mtaalamu wa hali ya hewa  Bw. Wilberforce Kikwasi akifanya mahojiano na mwandishi wakati wa maadhimisho ya siku ya bahari Afrika  yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ubaharia (DMI), Dar es Salaam, tarehe 24 mpaka 26 Julai 2019
Mtaalamu wa hali ya hewa  Bw. Wilberforce Kikwasi akiwasilisha mada kwenye kongamano la wadau wa sekta ya bahari lililoandaliwa wakati wa maadhimisho ya siku ya bahari Afrika  yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ubaharia (DMI), Dar es Salaam, tarehe 24 mpaka 26 Julai 2019

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA INAWAKARIBISHA WANANCHI WOTE KATIKA MAONESHO YA NANENANE, 2019


Tuesday, July 23, 2019

TMS YAWA CHACHU KATIKA KUFANIKISHA MALENGO YA TMA KWA KUCHOCHEA MATUMIZI SAHIHI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA SEKTA MBALIMBALI HAPA NCHINI.

Washiriki wa mafunzo yaliyofanyika katika hamashauri ya mji Bariadi, Simiyu kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhandisi Masha Luhamba ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. (wa pili kutoka kulia kwa waliokaa)
Matukio mbalimbali kwa picha wakati sekta mbalimbali zikijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika hamashauri ya mji Bariadi, Simiyu.
Matukio mbalimbali kwa picha wakati waandishi wa habari wakijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika Halmashauri ya mji Bariadi, Simiyu












Picha mbalimbali za matukio wakati sekta mbalimbali zikijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika mkoa wa Tanga.














Waandishi wa habari kwenye picha ya pamoja na Rais wa TMS, Dkt. Buruhani Nyenzi (katikakati ya waliokaa) waliposhiriki mafunzo ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika mkoa wa Tanga. Picha nyingine ni matukio mbalimbali wakati mafunzo hayo yakiendelea.


Chama cha Wataalam wa Hali ya Hewa Tanzania (TMS) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kimeendelea kukutana na wadau toka sekta mbalimbali wa kilimo, mifugo, nishati, maafa, maji pamoja na wanahabari kwa mikoa ya Tanga tarehe 01- 02 Julai2019  na  Simiyu  tarehe 08- 09 Julai 2019,  katika kuwajengea uwezo wa kutumia taarifa za hali ya hewa kwa usahihi. Hii ni katika muendelezo wa utekelezaji wa mradi “Weather and Climate Information Services” (WISER II)

Katika ufunguzi wa warsha iliyofanyika Simiyu, Rais wa TMS Dkt. Buruhani Nyenzi aliwashukuru wadau wote kwa ushiriki wao na kuendelea kuwasisitiza kufuatilia na kutumia taarifa za hali ya hewa katika shughuli zao za kiuchumi.

Aidha Mgeni rasmi Mhandisi  Masha Luhamba ambaye pia ni Kaimu katibu tawala Mkoa Simiyu  alihamasisha washiriki kuzingatia mafunzo hayo,  ambayo anaamini yatasaidia kufikia malengo ya kimkoa katika kuifanya Simiyu kuwa ya viwanda katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Serikali ya awamu ya tano Mhe. John Pombe Magufuli yenye lengo la kutufikisha kwenye uchumi wa kati na viwanda. 
 “naomba mtambue kuwa mmechaguliwa ninyi kati ya watendaji wengi wa serikali hapa mkoani Simiyu hivyo  nina imani kubwa sana toka kwenu ya kuwa mabalozi wazuri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania hapa Simiyu kupitia mafunzo mtakayoyapata na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za hali ya hewa kwa wakati na kuzielewa ili kusaidia kuongeza tija katika uzalishaji malighafi ambazo zitatumika katika viwanda na kufanya mkoa wetu uwe wenye viwanda vya kutosha” alisema Mhandisi Luhamba.

Pia warsha hiyo ilifanyika katika mkoa wa Tanga, ambapo washiriki waliahidi kuisambaza elimu hiyo waliyoipata kwa wadau kutoka katika sekta zao hususani wavuvi  ili wawe na mazoea ya kufuatilia utabiri wa hali ya hewa kabla ya kuingia Baharini. 


IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...