Tuesday, June 11, 2019

NDITIYE: WMO INAMCHANGO MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA TANZANIA.

Mhe. Atashasta Nditiye akihutubia mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
Mhe. Atashasta Nditiye akiwa na kaimu Balozi  Bw. Robert Kahendaguza, mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi na baadhi ya waumbe kutoka Tanzania
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)



Na: Christopher Philemon, Monica Mutoni. Geneva
11/06/2019.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye ameeleza namna ambavyo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linavyochangia katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania.  Mhe. Nditiye alizungumza hayo wakati akihutubia mkutano wa 18 wa WMO, unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.

‘WMO ina mchango mkubwa katika huduma za hali ya hewa nchini kama vile miongozo maalum iliyowekwa kwa ajili ya uandaaji na utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya ziwa Viktoria ambapo TMA inatoa miongozo ya tahadhari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, utekelezaji wa Mfumo wa Kidunia wa Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services-GFCS) ambao ndani yake Tanzania kupitia TMA inanufaika masuala mbalimbali kama vile mafunzo ya muda mrefu na mfupi, upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa n.k’ alisema Mhe. Nditiye.

Aidha, katika hotuba yake, Mhe. Nditiye aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuelezea namna serikali inavyoweka jitihada kubwa kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za kisasa kwa kufanikisha ununuzi wa rada tatu za hali ya hewa pamoja na kuifanya TMA iweze kukidhi zaidi matakwa ya watumiaji kwa kuibadilisha TMA kutoka kuwa Wakala na kuwa Mamlaka kamili.

Wakati akimalizia hotuba yake, Mhe. Nditiye alitumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii nchini na kumnadi mgombea wa nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi kutokana na uwezo na uzoefu alionao WMO akiwa mjumbe wa kamati kuu wa shirika hilo kwa miaka saba.  

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...