Tuesday, June 4, 2019

TMS YAONGEZA JITIHADA ZA KUWAJENGEA UWEZO WADAU WA SEKTA MBALIMBALI NA WANAHABARI JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NCHINI.





Washiriki wa mafunzo yaliyofanyika katika halmashauri ya mji wa Dodoma mjini kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi mh. Godwin Kunambi (mwenye suti nyeusi, wapili kutoka kulia). Picha nyingine ni matukio mbalimbali wakati mafunzo hayo yakiendelea.



Matukio mbalimbali kwa picha wakati Sekta mbalimbali zikijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika halmashauri ya mji wa Kongwa









Washiriki wa mafunzo yaliyofanyika katika halmashauri ya mji wa Hanang' kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi ndg. Liberatus Msasa (katikati mwenye koti la suti ya kijivu) kulia kwake ni mwakilishi wa rais wa Chama cha Wataalam wa Hali ya Hewa Tanzania (TMS) ndg. Philbert Tibaijuka na kushoto kwake ni bi. Elva Mziho meneja wa kituo cha hali ya hewa Babati. Picha nyingine ni matukio mbalimbali wakati mafunzo hayo yakiendelea.





Matukio mbalimbali kwa picha wakati waandishi wa habari  wakijengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika halmashauri ya mji wa Babati

Chama cha Wataalam wa Hali ya Hewa Tanzania (TMS) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia mradi wa Weather and Climate Information Services” (WISER), WISER, kiliweza kuwajengea uwezo wadau wa sekta mbalimbali (Kilimo, ufugaji, nishati, maafa, maji pamoja na wanahabari) katika halmashauri za miji ambazo ni Kongwa, Dodoma mjini, Hanang’ na Babati kwa kuendesha mafunzo ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kuanzia tarehe 27 Mei mpaka 31 Mei 2019.


Wageni rasmi katika mafunzo hayo, walikuwa ni wakurugenzi wa halmashauri za miji ambao katika hotuba zao waliishukuru TMS kwa kuchagua kufanya mafunzo hayo muhimu katika halmashauri zao. Aidha, wageni rasmi walihamasisha kila mshiriki kupitia taaluma zao kuitumia vyema fursa hiyo adhimu waliyoipata kwa kutambua namna ya kupata taarifa za hali ya hewa, kuzielewa kwa usahihi na pia kuzifikisha kwa walengwa kwa wakati zitakazoimarisha mchango wa sekta ya hali ya hewa katika kuongeza tija na ufanisi kwenye kilimo ambacho kina mchango mkubwa wa kuzalisha malighafi kwa ajili ya Tanzania ya viwanda hivyo utekelezaji wa programu hii utachangia katika kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli za kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati na uchumi wa viwanda.


Kwa upande wa washiriki walikiri kupata uelewa kwa kiasi kikubwa  na kuahidi kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinatumika kwa usahihi na kusambazwa kwa wakati ili kuwafikia walengwa pamoja na  kuweka nguvu kubwa katika kushirikiana na TMA.


Malengo ya mafunzo hayo ni kuchochea matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa sekta mahsusi zilizoainishwa katika mradi wa WISER na kuwafikia wananchi wengi kupitia huduma ya taarifa za hali ya hewa inayotolewa kwa njia ya simu za mikononi uitwao FarmSMS, ambapo zaidi ya wadau 600 walisajiliwa katika mfumo huo.



IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

2 comments:

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...