Sunday, June 30, 2019

NDUGAI AFURAHISHWA NA UCHAPAKAZI WA DKT. KIJAZI


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Pembeni ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi. Atashasta Nditiye. Dkt. Kijazi alishinda nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Juni, 2019 Geneva, Uswisi.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi. Atashasta Nditiye
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi (kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi. Atashasta Nditiye walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Dkt. Kijazi alishinda nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Juni, 2019 Geneva, Uswisi
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi (wanne kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi. Atashasta Nditiye. Dkt. Kijazi alishinda nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Juni, 2019 Geneva, Uswisi.
Ugeni kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi (watano kulia) walipotembelea  Bungeni Jijini Dodoma tarehe 28 Juni 2019. Dkt. Kijazi alishinda nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Juni, 2019 Geneva, Uswisi.

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ameonesha kufurahishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi.

‘Utendaji wako wa kazi ni wa kiwango cha juu, tunaona mafanikio ya TMA katika utoaji wa taarifa za hali ya hewa nchini kwa usahihi zaidi kulinganisha na huko nyuma ’ Alizungumza mhe. Ndugai

Mhe. Ndugai aliendelea kwa kumpongeza Dkt. Kijazi kwa kuchaguliwa kuwa makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwani imeonesha kazi kubwa inayofanywa na  TMA chini ya uongozi wake hivyo kumpa nafasi ya kushinda kwa kishindo na kuiletea sifa nchi katika nyanja za kimataifa.

Katika hatua nyingine, wabunge wa Bunge la JMT walimpongeza Dkt. Kijazi kwa shangwe kubwa mara alipotambulishwa ndani ya Bunge hilo na Mhe. Spika kama makamu wa tatu wa Rais wa WMO. Wabunge walionekana wakishangilia kwa furaha kuashiria kukubaliana na pongezi zilizokuwa zinawasilishwa na mhe. spika kwa niaba ya wabunge wote kabla ya kuahirisha rasmi vikao vya bunge la bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20

Naye, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipata wasaa wa kuliambia Bunge jinsi mchakato wa uchaguzi ulivyoenda na umuhimu wa nafasi hiyo ya juu kwa TMA, Tanzania na Afrika, sambamba na kulishukuru Bunge kwa ushirikiano waliouonesha katika kampeni za awali wakiwakilishwa na Mhe. Mboni Mhita , mbunge wa Handeni Vijijini.

Dkt. Kijazi alikutana na Mhe. Spika na kuhudhuria Bunge kupitia mwaliko wa Mhe. Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano uliokuwa na lengo la kumtambulisha mteule wa nafasi ya makamu watatu  wa Rais wa WMO kutoka Tanzania na kutoa shukrani za ushirikiano wa Bunge hilo. Aidha, Dkt. Kijazi alimshukuru Mhe. Spika kwa pongezi na kuahidi kuongeza juhudi katika utekelezaji wa majukumu ya TMA na WMO ili kuendelea kuiletea heshima nchi katika sekta ya hali ya hewa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA)
(Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge)

Friday, June 28, 2019

BODI YAMPONGEZA DKT. KIJAZI KUCHAGULIWA MAKAMU WA TATU WA RAIS WA WMO







Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imempongeza Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa hiyo kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Akizungumzia pongezi hizo na ushindi uliopatikana wakati wa kikao cha 55 cha Bodi, mwenyekiti wa Bodi Dkt. Buruhani Nyenzi aliwasilisha pongezi za dhati kutoka kwa wajumbe wote na kukiri kuwa nafasi iliyopatikana ni moja ya njia za kuzidi kuipandisha Tanzania juu katika anga za kimataifa.

‘Bodi inatoa pongezi za dhati kwa Dkt. Kijazi kwa kuchaguliwa kushika nafasi ya juu WMO, kwa kuwa kupitia nafasi hiyo Tanzania inazidi kupanda juu katika anga za kimataifa’. Aliongea Dkt. Nyenzi

Mwenyekiti huyo aliendelea kuwakumbusha washiriki wa kikao hicho kuwa mafanikio ambayo Tanzania imeyapata yanachangiwa na mambo mengi. Alisema jambo la kwanza na la muhimu ni sifa za Dkt. Kijazi kama mgombea wa nafasi hiyo, pili kukubalika na kukua kwa diplomasia ya Tanzania nje ya nchi na tatu sifa nzuri za Watanzania ambao wamewahi kufanya kazi WMO akiwemo yeye mwenyewe.

Aidha, Dkt. Nyenzi alionesha furaha yake namna ambavyo TMA inafanya kazi kwa umoja na upendo baina ya wafanyakazi, akitolea mfano mapokezi yaliyofanywa na wafanyakazi kwa kiongozi wao ambaye ni Dkt. Kijazi.

Dkt. Kijazi alichaguliwa kuwa makamu wa tatu wa Rais wa WMO kwenye mkutano wa 18 wa shirika hilo uliofanyika jijini Geneva, Uswisi tarehe 03-14 Juni 2019 kwa kipindi cha miaka minne, akiwa mwanamke na makamu wa tatu wa Rais wa kwanza kutoka nchi zinazoendelea hususani nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

IMEANDALIWA NA;
OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA)

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...