Thursday, October 4, 2018

TMA YATOA ELIMU YA HALI YA HEWA KATIKA KUULINDA NA KUUTUNZA URITHI WA NCHI YETU

Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wamejumuika katika kuadhimisha mwezi wa Urithi Festival kwa mkoa wa Dar es Salaam yanayofanyika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama Tarehe 01 hadi 06 Oktoba 2018.

Katika maonesho hayo  TMA ambayo ni taasisi iliyopewa jukumu la kutoa huduma za hali ya hewa nchini imeendelea kutoa elimu namna ya kuulinda na kuutunza urithi wa nchi yetu kwa kutambua faida za matumizi ya taarifa za hali ya hewa.

Miongoni mwa elimu inayotolewa ni matumizi ya taarifa za hali ya hewa za muda mfupi, kati,  mrefu na takwimu  za hali ya hewa katika kulinda mali kale mfano majengo ya zamani yaliyo kando ya fukwe za bahari ambapo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa/tabia nchi utafiti unaonesha uwepo wa ongezeko la kina cha bahari hivyo kupelekea uwezekano wa kupotea kwa urithi wa nchi hii. Aidha kuhamahama kwa wanyama kutokana na kutafuta malisho, ikumbukwe kuwa uoto wa asili hutegemea hali ya hewa nzuri kama vile mvua za kutosha

Vilevile, kwa upande wa kilimo watanzania wana shauriwa kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinafuatwa ili kuweza kuendelea kulima na kuzalisha mazao ya asili kwa jamii. Pamoja na hayo TMA pia hutoa taarifa za hali ya hewa zinazosaidia kuchagua vazi la asili la kuvaa kwa kipindi husika kama vile baridi, joto n.k

Ngoma na michezo ya asili pia hutegemea hali ya hewa ya eneo husika kama vile upepo mkali, mvua kubwa kwa maeneo ya michezo ya ziwani, viwanjani n.k

TMA inawakaribisha wananchi wote kufika katika banda lake ili kuweza kujifunza mengi yanayohusu hali ya hewa na maliasili na utalii (urithi wetu)


IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...