Thursday, October 11, 2018

TMA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MVUA ZA MSIMU WA NOVEMBA 2018 HADI APRILI 2019

Pichani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a akifungua rasmi warsha iliyowajumuisha wataalamu wa hali ya hewa TMA na wadau toka Sekta mbalimbali kujadili mvua za msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019

Mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA akiwasilisha mada



Pichani ni wadau kutoka katika sekta mbalimbali wakitoa maelezo ya mchango wa taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao.






Pichani ni Makundi mbalimbali yakijadili namna wanavyoweza kuutumia Utabiri wa Hali ya Hewa katika utekelezaji wa majukumu katika sekta mbalimbali hapa nchini na baadae kuwasilisha kwa wajumbe
Katikati ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa dkt. Ladislaus Chang'a kwenye picha ya pamoja na washiriki kwenye warsha ya wadau kutoka sekta mbalimbali walipokutana na wataalamu wa hali ya hewa kujadili mvua za msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019  


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo tarehe 11/10/2018 imekutana na wadau kutoka sekta ya maafa, afya, kilimo, nishati, mazingira,mipango miji na wanahabari kujadili matarajio na mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 ili kuongeza uelewa wa taarifa za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali zinazoathirika zaidi na hali ya hewa.

Aidha, wadau walipata nafasi ya kujadili mwenendo wa utabiri wa msimu wa vuli (Oktoba hadi Desemba 2018) uliotolewa 05 Septemba 2018 ambao unaonesha kuwa mvua zimeanza (onset) kama ilivyotabiriwa kwa maeneo mengi ingawaje mtawanyiko wake bado haujaimarika hali inayosababishwa na mgandamizo mdogo wa hewa uliopo Mashariki mwa Pwani ya Somalia unaoathiri mifumo ya hali ya hewa

Kwa upande wa mdau kutoka wizara ya afya bw.Stephen Kiberiti aliwashukuru TMA kwa utaratibu wa kukutana na wadau hii inasaidia sekta husika kujiandaa na athari zinazoweza kujitokeza.

Mikoa inayopata mvua mara moja kwa mwaka ni Dodoma, Singida, Katavi, Mbeya,Tabora, Kigoma(ukitoa Kigoma Kaskazini), Mtwara, Lindi,Ruvuma, Iringa, Songwe, Rukwa, Njombe na Kusini mwa Morogoro

Warsha hii imedhaminiwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kupitia mradi wa mfumo wa kidunia wa huduma za hali ya hewa Duniani (Global Framework for Climate Service-GFCS)

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...