Wednesday, September 19, 2018

DKT.KIJAZI ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KUFANIKISHA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KIDUNIA YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA AWAMU YA PILI.


Tarehe 17 Septemba 2018; Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wameshirikiana katika kuandaa kikao kazi cha kwanza cha utekelezaji wa programu ya kidunia ya huduma za hali ya hewa kwa awamu ya II. Kikao kazi hicho kilifanyika katika ukumbi wa mkutano uliopo Golden Jubilee, Dar es Salaam. 

Malengo ya kikao kazi hicho ni kupitia taarifa za utekelezaji wa awamu ya kwanza ya programu ya kidunia ya huduma za hali ya hewa ili kutambua mafanikio yaliyopatikana, changamoto zake na namna ya uboreshaji wa utekelezaji wa awamu ya pili katika kufanikisha malengo ya awamu ya pili. Programu ya Kidunia ya huduma za hali ya hewa awamu ya pili imedhaminiwa na shirika la misaada la Norway (Norwegian Agency for Development Cooperation (NORAD)) na kutekelezwa na nchi ya Tanzania na Malawi pekee kwa nchi za Afrika.

Akifungua kikao kazi hicho katika hotuba ya Dkt. Agnes Kijazi, mkurugenzi mkuu wa TMA na mwakilishi wa kuduma wa WMO kutoka Tanzania  iliyowasilishwa kwa niaba yake na mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya huduma za hali ya hewa, Dkt. Ladislaus Chang’a alisisistiza ushirikiano wa taasisi shiriki katika utekelezaji wa proramu ya kidunia ya huduma za hali ya hewa kwa awamu ya pili kwa vile umuhimu wake umeonekana wakati wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ambapo shughuli mbalimbali ikiwemo mipango na mikakati ya kufanikisha programu ilifanyika kwa ushirikiano wa pamoja. Aliongezea kwa kukitaka kikao kazi hicho kuhakikisha shughuli/mikakati ya utekelezaji wa awamu ya pili inaendana na malengo ya mfumo wa taifa wa huduma za hali ya hewa (NFCS). Malengo ya NFCS yalitokana na utekelezaji wa awamu ya kwanza katika kutambua changamoto zake.

Kikao kiliwajumuisha watendaji wa utekelezaji wa programu kutoka  Ofisi ya Waziri Mkuu (Kitengo cha Uratibu wa Maafa),), Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia na watoto, Wizara ya Kilimo, Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania pamoja na washiriki wengine kutoka Shirika la Halin ya Hewa Dunia (WMO) na Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC). Tanzania inatarajia kuzindua rasmi programu ya kidunia ya huduma za hali ya hewa kwa awamu ya pili, tarehe 18 Septemba 2018, katika ukumbi wa  Golden Jubilee Towers, Dar es Salaam.

Imetolewa:
Monica Mutoni,
Ofisi ya Uhusiano,
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...